Wolper adai amedhalilishwa na gazeti la Sani, ni baada ya kuandika ‘Wolper abakwa na msanii wa Diamond’

Wolper Mwigizaji huyo mahiri ambaye kwa sasa anatoka kimapenzi na msanii kutoka WCB, Harmonize, ameonyesha kuchukizwa na kitendo hicho na kuamua kuwashtaki kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es saalam, Paul Makonda.
Kupitia instagram, Wopler ameandia:
I am so sad kwakweli
Hii sio kuniabisha mimi tu, ni kuaibisha na wanawake wenzangu, sijui kwanini magazeti ya kibongo yanatumia Nguvu nyingi kushusha hadhi ya wasanii wa kike haswa.. Nyie SANI no wonder mmepotea katika soko.. Hivi mlivyokua mnachapa mmefkiria kuna wadogo zangu wanasoma?? Au mama angu na baba yangu!
Naandika kwa uchungu kwakua najua ni limtu limekosa kazi ya kutumia kipaji chake na karama yake vyema linaishia kutumia kwa kuniharibia maisha yangu… Tena front page? Tunafany mangapi mazuri hatuingii page ya kwanza hata siku moja,?! Kesho kutwa nafungua biashara mtaona kama wataandika kitu
Ila kwenye ujinga wa kutunga ndo wakwaza, Si mmeamua kuniandika mimi hivi!??!, na kila siku mnafanya hivi. My loves embu nisaidieni niwaambie nini cha zaidi wauaji kama hawa. Kuna uuaji wa aina nyingi… Hata maneno huua jamani, sisi pia tu a mioyo
Dah!

BIG SHAME ON YOU GUYS
Kuanzia alietunga stori, alieidhinisha ichapishwe na mwenye gazeti
Kwanini Mh @paulmakonda hawa wasiwe wanapigwa faini au hata kupelekwa mahakamani?? Manake msamaha hautoshi
Wanaharibu kabisa maana ya vyombo vya habari
Petty and sad
Stupid

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016