Baada ya tetesi za Naj kunasa ujauzito kusambaa,Barakah Da Prince ametamka haya.


Hit maker wa hit single ya ‘Siwezi’,Baraka Da Prince amekanusha tetesi zilizosambaa mitandaoni kuwa mpenzi wake ambae pia ni mwanamuziki,Naj Dattani kuwa na ujauzito hali iliyopelekea kukwama kwa mipango yake ya kuachia wimbo mpya.
naj dattani 0005
Baraka ambae ni mshindi wa tuzo za KTMA mwaka jana katika kipengele cha mwanamuziki anaechipukia,aliongeza kwa kusema kuwa alipanga kuachia kazi  mpya mwanzoni mwa Julai lakini ameshindwa baada ya kupata management  mpya na kwamba kwa sasa kuna baadhi ya mambo wanayaweka sawa hivyo anatarajia kuachia kazi mpya mwezi  Agosti mwaka huu. “kuhusu Najma kuwa mjamzito kwa kweli hizo taarifa sifahamu”…..”kama upo utaonekana tu maana hicho kitu huwa hakijifichi”.Alisema Da Prince.
barakah


Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016