VIDEO:MKUBWA FELLA afunguka kwa kina juu ya Mapenzi ya ASLAY na RUBBY

Said Fella amedai kuwa uhusiano wa siku moja na tena kwenye Instagram kati ya Aslay na Ruby ulikuwa kiki tu.
13257159_1025726880797930_1241785849_n
Akiongea na 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM, Fella alisema kuwa Aslay alitumia njia hiyo ili kupima mafuta kama kweli mashabiki wa Yamoto Band bado wapo ama wameshawachinjia baharini.
“Kilichofanyika kwa Aslay ni kwamba je nikisema kwamba mimi labda natoka na mtu fulani kwanza hakuwahi kusema anatoka naye ila watu ndio walikuwa wanatafsiri wao ‘mbona anampost huyu.’ Na sisi watu wengi kwenye Mainstagram haya tunatafsiri sana kuliko hata yule mlengwa aliyempost,” amesema Fella.
“Kwahiyo ilikuwa hivyo kujua je mashabiki wa Yamoto bado wapo? Na kweli wameonesha bado wapo na ndio maana nyimbo ndani ya kila chochoro yote Tanzania watu wamejua.”
Fella amesema kiki hiyo haijawa na athari yoyote kwao.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016