PICHA:Aliedaiwa kuwauzia watu nyama ya mmbwa mkoani Tanga ahukumiwa kifungo cha mwaka 1 jela.

Kijana aliyefahamika kwa jina la Zakaria Swaki, mkazi wa Kijiji cha Mlalo, wilayani Lushoto mkoani Tanga,yupo nyuma ya nondo za gereza la Lushoto akitumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja baada ya  kukutwa na hatia ya kuwalisha watu nyama ya mbwa na kukiri makosa yake mbele hakimu wa Mahakama ya mwanzo Mlalo,hali iliyozua  taharuki kwa wakazi wengi mkoani humo wakidai kuwa,kwa hali ilivyo watakuwa hawawaamini wauza nyama.
NYma ya mmbwa 0002         Zakaria Swaki,anaedaiwa kuwauzia watu nyama ya Mmbwa.
Kwa upande wake kamanda wa polisi Mkoani Tanga Leornad Paul,amewapongeza wananchi kwa kutoa ushirikiano hadi kufanikisha kukamwatwa kwa kijana huyo na kuwataka wananchi kuwa waangalifu hasa kuelekea katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kununua vitoweo hasa nyama kwenye ma-butcher yaliyoidhinishwa na kupata vibali vya maafisa afya wa wilaya.
Nyama ya mmbwa 002Wakizungumza  kwa nyakati tofauti, wananchi hao wa kijiji cha  Mlalo na viunga vyake walisema walikuwa wanatilia shaka nyama aliyokuwa akiuza kijana huyo ambapo taarifa zidai kuwa  alianza kufanya mchezo huo  muda mrefu,“Kwa kweli nimeshitushwa sana na taarifa hii, sina hata hamu ya kula tena nyama maana inavyoonekana amewauzia watu nyama hiyo kwa muda mrefu,” alisema Jamali Shemshahuo, mkazi wa Kijiji cha Ngazi.
Nyama ya Mbwa 003“Niliwahi kununua nyama kwa yule kijana lakini niliitilia shaka licha ya kwamba niliipika na kuwauzia wateja wangu na wapo walioisifia supu yake kuwa ni tamu, kumbe maskini nilikuwa nawalisha watu nyama ya mbwa”.Alisema Mama Jenny,anaefanya biashara ya kuuza vinywaji na chakula eneo la Misheni mkoani Tanga.
Credit : Globalpublisher.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016