Watuhumiwa ubakaji na usambazaji picha za binti wa miaka 21 wafikishwa kortini chini ya ulinzi mkali

Watuhumiwa wawili wa tukio la ubakaji lililotokea Morogoro, Jumatano hii walipandiswa kizimbani kwenye mahakama ya mkoani humo.
13166801_1632014527124402_853971816_n
Wawili hao Idd Adam Mabena wa Njombe, Zuberi Thabiti wa Mbarali wanadaiwa kutenda kosa hilo April 27 usiku kwenye nyumba ya kulala wageni. Hata hivyo washtakiwa hao wamekana makosa yao na hivyo kesi hiyo itasikilizwa tena June 1.
Upande wa mashtaka pia umewasilisha kiapo cha pingamizi la dhamana kwaajili ya usalama wa washtakiwa hao kutokana na tukio lao kugusa hisia ya jamii.
Washtakiwa hao na wengine wanne waliokamatwa kwa madai ya kusambaza picha chafu za tukio hilo wamerudishwa rumande.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016