Sababu ya Kifo cha Msanii wa uchekeshaji "KINYAMBE" alikuwa na Uvimbe tumboni

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania kutoka katika Kundi la Vituko Show, Mohammed Abdallah ‘Kinyambe’ amefariki dunia Jumatano hii baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na uvimbe tumboni. 1
Taarifa za kifo chake zilianza kuzagaa jana katika mitandao ya kijamii baada ya wasanii wa filamu kuanza kupost picha mbalimbali huku wakiandika RIP Kinyambe.
Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii mmoja kati ya wasanii wanaounda Chama Cha Wasanii Wachekeshaji Tanzania, Mkono Mkonole, amesema Kinyambe amefariki jana akiwa mkoani Mbeya.
“Kinyambe alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni kwa muda mrefu, ila jana ndo amefariki akiwa mkoani Mbeya, katika hospitali ya mkoa wa Mbeya,” alisema Mkonole.
Kuhusu taratibu za mazishi, Mkonole amesema bado hawajapanga kwani taarifa za kifo chake wamezipokea jana usiku.
“Kusema kweli bado hatujapanga kuhusu mazishi, lakini sasa hivi tunawasiliana na ndugu zake ili kujua taratibu za mazishi na zikamilika tutaweka wazi,” alisema Mkono.
Kinyambe atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuigiza, hasa hasa jinsi anavyoongea pamoja na mtindo wake wa pekee wa kugeuza macho.
Baada ya taarifa hizo, wasanii mbalimbali wa filamu na muziki walishare ya moyoni jinsi walivyozipokea taarifa hizo za kusikitisha.
Riyama Ally

Innalilah wainna ilaihi rajiun mbele yake nyuma yetu kazi yake mola haina makosa mola akueke panapo stahili ndugu yetu Amin #kinyambe wasanii wenzangu rafiki zangu dunia na #dini dunia mapito #DUNIAMALIYAMUNGU BINADAMU #PUMZITU (TUPENDANDE TUHESHIMIANE) MUNGU NDIO KILA KITU . 😒😒😒😒😒😒😒😒😒😒😒😒😒😒

Raymond
Daaah!!!!! SIAMINI NINACHOKIONA.ULIKUA MTU POA SANA NAKUMBUKA ULIVYOKUA UKINISAPOTI MDOGO WAKO KITAMBO SANA.KAZI YA MOLA HAINA MAKOSA. R.I.P BROTHER MUDI #KINYAMBEa

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016