Picha za ndoa yaMsanii LUTENI KARAMA baada ya kumpiga chini ISABELA amuoa mrembo huyu

Msanii wa muziki aliyewahi kutamba na Kundi la Gangwe Mob, Luteni Karama ambaye kwa muda mrefu anafahamika kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Isabela Mpanda, Jumamosi iliyopita alimuacha kwenye mataa na kufunga ndoa na mrembo Aisha Yassin, Mkazi wa Magomeni Mikumi jijini Dar. kkkss
Shughuli hiyo ilianza mapema, lakini ilipotimu saa tisa jioni, umati ulikusanyika nyumbani kwa mrembo huyo kumshuhudia nyota huyo wa Bongo Fleva akikabidhiwa ‘kifaa’ hicho ili kuanza maisha mapya ya ndoa.
Kupitia instagram, Luteni aliandika:
Raha ya mapenzi ni kupendana na kuheshimiana na Mola kanijaalia mke mwenye vyote hivyo Mungu akuzidishie mke wangu @official_mrskarama na maneno ya watu usiyaskilize binadamu hawana jema wewee mapenzi yana siri yake wacha mwingu watu waendele kuhukumu ukweli tunaujua wenyewe Aisha mke wa maisha yangu
kkk kkkss
kkkss

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016