Gigy money kuachia video ya wimbo ‘Tikisa Supu’, ataka watoto wakae mbali...Cheki Video

Msanii wa muziki, Gigy Money anatarajia kuachia video yake mpya ya wimbo ‘Tikisa Supu’, ambapo amewataadharisha watoto kukaa mbali na kazi hiyo.
Muimbaji huyo ambaye pia ni video queen, ameiambia Ijumaa hii kuwa ameamua kuachia wimbo ‘Tikisa Supu’ baada ya kuona tayari kuna watu wengi ameshaimba nyimbo za kutikisa sehemu za miili yao.
“Unaniuliza kucheza, nitikise nini?, maana watu wameshatikisa kiuno, mapaja, nitikise matiti?, no, hawataki. Nitikise Supu, wanataka. Kwa hiyo kwa lugha za kwenye runinga nikisema nitikise makalio haitaleta picha nzuri, na nyimbo naihisi itapendwa sana,” alisema Gigy.
Video ya wimbo ‘Tikisa Supu’ utatoka katikati ya mwezi huu baada ya kukamilika kwa matayarisho ya mwisho.
<!-- adsense

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016