FAHAMU:Aina ya mazoezi inayotumiwa na wanawake kutengeneza shepu nzuri

Kwanini uvae nguo za ndani zilizo na makalio ya upepo, wakati una nguvu na wewe bado kijana, kwanini uangaike kununua madawa ya kichina yalio na madhara kemkem katika afya yako.  Najua wachache wana uwezo wa kufanya  upasuaji kwa kuweka maumbile mengine  (plastic surgery) lakini pia sio salama.
Kupata mwili kama wa Nick minaj, inawezekana kwa kujituma  hasa kwa mazoezi, mazoezi aina ya squat ni mazoezi ambayo yanaweza kukufanya ukawa na shape ya kupendeza kama utafanya kwa kufwata maelekezo  na kuzingatia kanuni za mazoezi hayo.
Squat haikusaidii tu kutengeneza shape kama makalio pekeake ila pia husaidia kushape miguu yako, kusaidia kutoka minyama uzembe au (cellulite), mazoezi haya yanaweza ambatana na mazoezi ya kupunguza tumbo na kushape kiuno chako ili uwe na kiuno kama nyigu yaani chembamba.
firm-butt-squat 3
Nini cha  kufanya? Kwa wale wasio na uwezo wa kuwatafuta wataalamu wa mazoezi haya au kwenda Gym, unaweza kutumia Mitandao ya kijamii  kama Instagram kutafuta kurasa mbalimbali zinazoonyesha  mazoezi kwaajiri ya wadada pia wakitoa na ushauri pamoja na video mbalimbali ambazo unaweza ukafanya ukiwa nyumba iwe na vifaa au bilaa vifaa.
Matokeo baada ya kufanya mazoezi haya yanatokana na juhudi zako na najua watu wengi ni wavivu  na wanatamani matokeo ya haraka kitu ambacho hakiwezi kuwa raisi. Unaweza kutumia zaidi ya miezi mitatu kupata unachokifanyia kazi kwa bidii. Jiwekee ratiba yako ya mazoezi kwa dakika 15 tu kila siku na unaweza kuona matokeo.
deep-squats-2
Unaweza pia kufanya kama ni tamaduni yako kukimbia na kufanya mazoezi mengine ya mwili kwani huwezi kutengeneza tu shape kama huna afya nzuri hii nikiwa na maana ukiwa mfanya mazoezi zingatia mlo wako na kunywa maji mengi, matunda na mboga za majani. Jenga shepu yako na mazoezi na sio madawa.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016