Baada ya “Shika adabu yako”kufungiwa Ney wa mitego amtumbua Shilole,Nisha na Wolper

Msanii wa Bongofleva anaongoza kwa kuwa na dis-tracks hits,Ney wa Mitego ameendelea kutupa vijembe kwa wasanii wa filamu nchini (Bongo Movie) and this time around mbongofleva huyo kupitia video clip aliyopost kwenye account yake ya instagram amewataja warembo kutoka Bongo Movie ambao wamekua wakijingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na wasanii wa bongofleva hasa wale wanaochipukia na single zao kufanya vizuri.
wa miteeeego 0004 “Kule bongo movie wasichana ambao huwa wanakwaruaga vichipukizi…kuna Wolper,kuna Nisher na Shilole….yaani wakisikia tu underground anafanya vizuri washamdaka”anasema Ney.
Staa huyo ambae anafanya vizuri na video yake ya “Saka Hela”haijafahamika kama yupo mbioni kuachia distrack nyingine inayowahusu warembo wa Bongo Movie ambao amekua akiwaandama kwenye nyimbo zake,ikiwa ni baada ya dis track yake ya “Shika adabu yako”kufungiwa na baraza la sanaa nchini (Basata)kutokana na wimbo huo kushutumiwa kuwa na mashairi ya udhalilishaji.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016