Wolper aogopa kuweka wazi zaidi mahusiano yake ya mapenzi

Akizungumza katika kipindi cha Nirvana cha East Africa Television Jumanne hii, Wopler alisema mpenzi wake wa sasa ambae alivalisha pete siyo mume wa mtu kama watu wanavyodai.
“Mimi sipendi kuzungumzia masuala ya mahusiano yangu na mchumba wangu kwenye vyombo vya habari,” alisema Wolper.”Kwani huweza kutokea mtu akaishia kwenye ‘engagement ring’ hivyo nitasema nikashaolewa na siyo sasa,”
Pia Wiopler alisema kwamba mchumba aliye naye kwa sasa alianza kumtongoza toka mwaka 2012 akakataa ila mambo yalivyoenda ndivyo sivyo kwa mchumba wa awali ikabidi amsikilize huyu ambaye yupo naye kwa sasa.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016