Ndugu wa Marehemu Sajuki Afungukia Talaka ya wastara Aliyopewa na Mbunge Zanzibar...

KUTOKANA na madai ya kupewa talaka na mumewe Sadifa Juma, ndugu wa aliyekuwa mume wa Wastara Juma, marehemu Sadick Kilowoko ‘Sajuki’, Mohamed Kingochi ‘Mdidi’ amefunguka kuwa ameumizwa na suala hilo kwani walitegemea ndiyo amepata mtu wa kumpa faraja.

Akipiga stori na paparazi wetu, Mdidi alisema wakati Wastara anaolewa walihuzunika ila siyo kwamba hawakutaka aolewe bali ni kutokana na mazoea kwamba watakosa kuwa naye karibu.

“Madai ya talaka ya Wastara yameniumiza sana kwani tulikuwa tunatatarjia akishakaa vizuri kwenye ndoa tuendeleze Kampuni ya WAJEY lakini tangu ameolewa, mambo ni vululuvululu na hili la talaka nalo ndiyo linazidi kutuumiza,” alisema Mdidi.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016