Baada ya Kukaa REHAB Mwezi ....Afya ya CHID BENZ Yaimalika


BAADA ya kumaliza mwezi mmoja akipata matibabu, afya ya rapa Chid Benz imeendelea kuimarika kila kukicha kufuatia tiba anayoendelea kuipata katika Kituo cha Rehab Bagamoyo. Kalapina amepost short clip video ikionesha hali ya rapa huyo akiwa anaendela vyema.
chidi
Alichokisema Chid Benz “Sina mengi ya kuongea, niko poa niko okay, niko sawa yani niko fresh na msaada ninaupata vizuri, na ninaendelea vizuri.”
Meneja wa Diamond, Babutale akishirikiana Kalapina walimpeleka Chidi Benz kwenye Kituo cha Life and Hope Rehabilitation Organization kilichopo Bagamoyo kwa ajili kumsaidiwa kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.
Hatua hiyo ilikuja baada ya rapa huyo kuomba msaada baada ya kuona ameshindwa kukabiliana na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakimkabili.
Watanzania tuendelee kumuombea Chid Benz ili afya yake iendelee kuimarika na hatimaye apone kabisa na mwi8sho wa siku tujiunge naye katika ujenzi wa Taifa letu.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016