Wafungwa wa kike Segerea ni wadada wa kazi

Mbunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Mh Bonnah Kaluwa amesema kuwa idadi kubwa ya wafungwa wa kike walipo kwenye gereza la Segerea ni wafanya kazi wa ndani alimaarufu kama (House Girls).
Mbunge wa Segerea
Kupitia mtandao wake wa Facebook mbunge huyo amesema kuwa alipotembelea gereza hilo juzi alishuhudia wingi wa wafungwa hao wa kike ambao wenngi wao wamefanya makosa madogo madogo kama ya kuchana dela la boss, upotevu wa vitu vya ndani, kupoteza fedha za matumizi.
"Juzi nilitembelea gereza la Segerea kujionea hali halisi na moja ya kitu nilichokishuhudia ni wingi wa wafungwa wa kike ambao wengi walikuwa wafanyakazi wa ndani (house girls). Nilipowauliza niligundua wengi makosa yaliyosababisha watiwe hatiani ni madogo kama kuchana dela la boss, upotevu wa vitu vya ndani, kupoteza hela ya mboga nk. Kwa ujumla makosa mengi yanafanana." Alisema Bonnah Kaluwa.
Kwa upande wake mbunge huyo aliwataka wanawake hususani maboss wa hao madada wa kazi kuyamaliza masuala hayo kwenye ngazi ya familia au kuwaruhusu tu warudi makwao pale wanapogundua wamefanya makosa fulani kuliko kwenda kuwafunga na kuwataka kuwa na moyo wa utu kwani anadai kwa muda ambao watakaa gerezani hawatajifunza zaidi watazidi kuwa sugu na kujifunza tabia nyingine mbaya zaidi.
"Mimi sio mwanasheria lakini naamini vitu kama hivi tunaweza kuvimaliza kwenye ngazi ya familia, nafahamu madada wengi wa kazi tunawatoa mikoani na baadhi hapa mjini, wana familia na ndugu ambao kutokana na kipato cha chini wamewaruhusu wajitafutie kipato cha kuwasaidia wao na familia. Kuna ugumu gani wa kumwambia arudi kwao unapogundua makosa ambayo hayasameheki? Kosa kama la kupoteza hela unashindwaje kumkata hata mshahara hadi itakapotimia?" Alihoji Bonnah Kaluwa
Aliongezea kwa kuwasihi kuwa "Nawasihi kina mama wenye madada wa kazi tujitahidi kuwa na moyo wa utu, kumbuka miezi sita au mwaka anaomuweka gerezani haumsaidii zaidi ya kumfanya awe sugu na kujifunza tabia nyingine mbaya. Tusiutumie vibaya msemo wa asiefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, tukumbuke mara unapoamua kuishi nae wewe ndiye unageuka mzazi wake wa pili hivyo unawajibu wa kumtunza kama mwanao na usisahau wazungu walisema "what goes around comes around" leo kwa mtoto wa mwanamke mwingine na kesho yatamkuta mwanao wa kumzaa". Alimaliza Bonnah Kaluwa.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016