Kauli ya Kwanza ya Diamond juu ya kumpima Tiffah DNA

Mkali wa muziki wa Bongo fleva hapa nchini, Nasib Abdul aka Diamond Platnumz, amekanusha tetesi zakwenda kumpima mtoto wake Latiffah 'Tiffah' vinasaba 'DNA' ili kupata uthibitisho wa kuwa ni mwanawe au sio mwanae.
Mwanamuziki wa Bongo fleva Nasib Abdul aka Diamond Platnumz
Diamond amezungumza hayo baada ya kufanyiwa mahojiano na eNewz kuhusiana na tetesi hizo ambapo alikanusha suala hilo, Diamond Anasema kumpima mtoto wako DNA ni kutojiamini na yeye hawezi kufanya hivyo, Diamond anasema alianza kumjua Tiffah akiwa tumboni.
Pia Diamond ameweka wazi kuwa picha inayomuonyesha akilia ni ya show yake ya Dar Live.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016