Nay wa Mitego "Siwema Hajawahi Kuja Kumuona Mtoto Wala Hata Kupiga Simu Kuulizia Hali ya Mtoto Tangu Nilipomchukua

Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego amesema kuwa mzazi mwenziye, Siwema hajawahi kumuona mtoto wao aitwaye Curtis wala kupiga simu kuulizia hali ya mtoto tangu alipomchukua kutoka kwake jijini Mwanza zaidi ya miezi miwili iliyopita.

Nay aliyazungumza hayo kwenye mahojiano maalum na Clouds FM kuhusu malezi ya upande mmoja anayolelewa mtoto wake Curtis mwenye umri wa miezi sita. ‘’Mtoto wangu anaendelea vizuri hana tatizo,na mama yake wala ndugu zake hawajawahi kumuona mtoto wala kupiga simu kuuulizia hali ya mtoto anaendeleaje,’ alisema Nay. ‘Na pia hali hiyo wala hainiumizi hata asipomuona miaka yote mimi sijali ninachoangalia mtoto wangu ana afya njema na anakua vizuri,’ aliongeza Nay.

Nay wa Mitego aliamua kumchukua mtoto wake kutoka kwa mama yake jijini Mwanza baada ya kutokea ugomvi kati yao.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016