KANUNI ZA KUFUATA ILI UWEZE ACHANA NA MPENZI WAKO

Upo uhusiano ambao umelengwa kudumu, hasa kwa wanandoa. Kuna wengine hawa sura ya kudumu, wapo kwa muda kwa kuzingatia mazingira pamoja na kile kilichomo ndani ya nafsi zao.

Unaweza kujiuliza; Kwanini ufike wakati utake kuvunja uhusiano wako na mwenzako? Iwe kirafiki au kimapenzi, Ipo wazi kwamba kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuwafanya wahusika kuamua.

Yawezekana uhusiano wako na mpenzi wako au rafiki yako wa jinsia tofauti unakutia hasara, au unakuharibia biashara, au unakupunguzia heshima katika jamii, au pengine uaminifu wako kazini. Mathalan, mpenzi wako anapokuwa anafahamika kuwa ni kahaba.

Inawezekana uhusiano wako na mwenzako unaidhuru nafsi yako. Mfano, mwenzio ana nguvu sana juu yako kiasi kwamba huwezi kusema “hapana” kwa lolote analokwambia. Pengine kutokana na hali hiyo umekuwa ukilazimika kufanya mambo ambayo huyapendi na ambayo hayaendani na maadili.

Lakini pia yawezekana umeanza kumchukia mwenzako. Mazingira yamebadilika, kwahiyo wewe na yeye hampatani tena. Unajitazama na kugundua kwamba ulivyo huendani naye. Ni matokeo ya kuchokana!

Naam, baadhi ya mahusiano, yawe ya kirafiki au kimapenzi, huwaweka katika wakati mgumu watu kiasi kwamba ni lazima mtu achukue hatua ili aweze kuishi kwa amani na furaha ya kweli. Hata hivyo, ikae akilini kwamba inauma mno kuachana na mtu unayempenda!

Kumaliza uhusiano wa kimapenzi au kirafiki si hatari, lakini la msingi ni kuhakikisha kuwa unamwacha mwenzako akiwa hajaathirika kisaikolojia kwa namna yoyote. Kwa sababu hiyo unapaswa kujifunza njia sahihi ya kumaliza uhusiano wako na mwenzako inapobidi.

Kuna jamii inaweza kuthubutu kusema, unapochoshwa na mtu, mchukue uende naye mahali kisha umueleze kwa uwazi kuwa hutaki tena kujihusisha naye kwa sababu moja, mbili, tatu. Hata hivyo, hilo si jambo rahisi kwa wengi.

Badala ya kukubaliana na mtu ana kwa ana na kumweleza kuwa humhitaji tena, zipo njia za kirafiki na za kidiplomasia ambazo unaweza kuzitumia na kumaliza mambo bila kusababisha matatizo makubwa au madhara yoyote ya kisaikolojia.

WEKA SABABU ZAKO MEZANI!
Unapotaka kumbwaga rafiki yako au mpenzi wako ambaye hujampa ahadi yoyote ya kuishi naye katika ndoa, anza mchakato kwa kuweka bayana sababu zinazokufanya utake kuachana naye. Hakikisha kuwa sababu unazoziweka ni zile ambazo mpenzi wako huyo hatapata namna ya kuzipinga.

Zitengeneze sababu hizo kwa kuzingatia mtazamo wako mwenyewe, na si kwa mtazamo wa mpenzi au rafiki yako huyo, ili hatimaye kusiwe na sababu ya mwenzako huyo kudhani atajirekebisha ili aweze kuendelea kuwa na wewe.

Namna hii utakuwa unayaangalia zaidi maslahi yako mwenyewe na iwapo utalazimika kumweleza mwenzako ni kwa nini unataka kumaliza uhusiano wako na yeye, sababu zako hazitaonekana kama shambulio kwake yeye mwenyewe wala tabia yake.

USITHUBUTU KUWASILIANA NAYE!
Utakapaokuwa umeweka wazi sababu zako na kuziamini, weka mkakati kuwa hutaanzisha tena mawasiliano na mwenzako. Jiwekee msimamo kuwa hutampigia simu, wala kumtumia ujumbe wa simu, wala baruapepe na kadhalika, ila utajibu tu yeye atakapoanzisha.

Unapomwalika mtu au kumpigia simu au kumtumia ujumbe ni kama unamtia moyo na kumfanya aamini kuwa unampenda na kumjali. Kama mhusika ni mtu mwenye fahamu atashtuka kuwa jitihada zote anafanya yeye na wewe uko kimya. Akitafakari atagundua kuwa hauko naye tena.

AKIKWITA KATAA!
Iwapo kweli umedhamiria kumaliza uhusiano wako na mwenzako, jaribu kukataa mialiko anayokupa, mathalani kwa ajili ya chakula cha pamoja cha mchana. Pia kama atasema atakufanyia jambo Fulani, kataa kiaina.

Fanya vivyo hivyo kwa matukio yote ya kijamii. Kataaa mialiko kwa njia ambayo hatkushtukia haraka kuwa humhitaji tena, bali aje kushtuka baadaye atakapojumlisha matukio.

Katika hatua za awali, hii itamaanisha kuwa utakosa kwenye matukio Fulani ambayo wewe mwenyewe ungependelea kuyahudhuria, lakini huna la kufanya, maana umeazimia kumaliza uhusiano wako na mpenzi au rafiki yako.

Unapotaka kupeleka ujumbe kwa mpenzi wako kuwa hayuko tena moyoni mwako, lazima tu ujitoleee kupata hasara katika baadhi ya mambo. Kumbuka kuwa huhitaji tena uhusiano wako na mwenzako.
WEKA SABABU ZAKO MEZANI!
Unapotaka kumbwaga rafiki yako au mpenzi wako ambaye hujampa ahadi yoyote ya kuishi naye katika ndoa, anza mchakato kwa kuweka bayana sababu zinazokufanya utake kuachana naye. Hakikisha kuwa sababu unazoziweka ni zile ambazo mpenzi wako huyo hatapata namna ya kuzipinga.

Zitengeneze sababu hizo kwa kuzingatia mtazamo wako mwenyewe, na si kwa mtazamo wa mpenzi au rafiki yako huyo, ili hatimaye kusiwe na sababu ya mwenzako huyo kudhani atajirekebisha ili aweze kuendelea kuwa na wewe.

Namna hii utakuwa unayaangalia zaidi maslahi yako mwenyewe na iwapo utalazimika kumweleza mwenzako ni kwa nini unataka kumaliza uhusiano wako na yeye, sababu zako hazitaonekana kama shambulio kwake yeye mwenyewe wala tabia yake.

USITHUBUTU KUWASILIANA NAYE!
Utakapaokuwa umeweka wazi sababu zako na kuziamini, weka mkakati kuwa hutaanzisha tena mawasiliano na mwenzako. Jiwekee msimamo kuwa hutampigia simu, wala kumtumia ujumbe wa simu, wala baruapepe na kadhalika, ila utajibu tu yeye atakapoanzisha.

Unapomwalika mtu au kumpigia simu au kumtumia ujumbe ni kama unamtia moyo na kumfanya aamini kuwa unampenda na kumjali. Kama mhusika ni mtu mwenye fahamu atashtuka kuwa jitihada zote anafanya yeye na wewe uko kimya. Akitafakari atagundua kuwa hauko naye tena.

KATAA ANAPOKUITWA
Iwapo kweli umedhamiria kumaliza uhusiano wako na mwenzako, jaribu kukataa mialiko anayokupa, mathalani kwa ajili ya chakula cha pamoja cha mchana. Pia kama atasema atakufanyia jambo fulani, kataa kiaina.

Fanya vivyo hivyo kwa matukio yote ya kijamii. Kataaa mialiko kwa njia ambayo hatakushtukia haraka kuwa humhitaji tena, bali aje kushtuka baadaye atakapojumlisha matukio.

Katika hatua za awali, hii itamaanisha kuwa utakosa kwenye matukio fulani ambayo wewe mwenyewe ungependelea kuyahudhuria, lakini huna la kufanya, maana umeazimia kumaliza uhusiano wako na mpenzi au rafiki yako.

Unapotaka kupeleka ujumbe kwa mpenzi wako kuwa hayuko tena moyoni mwako, lazima tu ujitoleee kupata hasara katika baadhi ya mambo. Kumbuka kuwa huhitaji tena uhusiano wako na mwenzako.

MUWEKEE MAPOZI
Kuna wakati ambapo rafiki au mpenzi wako atafanya au kusema jambo na wewe utatakiwa kuonesha mwitikio. Kama umeshadhamiria kuachana naye, onesha mwitikio wa shingo upande.

Kama mhusika atabaini jinsi ulivyoitikia shingo upande, utakuwa umepeleka ujumbe maridhawa, kwamba huna tena furaha na uhusiano wenu na kwamba unahisi ni wakati muafaka wa kumaliza mambo.

Kuna mazingira ambayo hutaepuka kumwitikia mpenzi au rafiki unayetaka kumpiga chini. Kwa sababu hiyo, ndiyo maana unapaswa kumwitikia lakini katika hali ambayo inaonesha kana kwamba huna habari naye sana.

Unapomwitikia mpenzi wako kwa shingo upande, unamwonesha kuwa si tena kipaumbele kwako, jambo ambalo litamfanya yeye mwenyewe kuona kuwa ni wakati muafaka wa kupunguza moto wake kwako.

KAA NAYE MBALI
Kama umekuwa na mazoea ya kuwa karibu na mpenzi wako kama ilivyo kawaida, anza kujenga mazingira ya kujitenga naye mnapokuwa mbele za watu, ili aweze kuhisi mabadiliko katika mwenendo wako.

Haina maana kuwa usizungumze naye kaa naye karibu na uzungumze naye kama kawaida, lakini majibu yako yawe ya mkato. Pia usikae karibu naye sana, maana namna hiyo utalazimika kuzungumza naye na kukaribisha lugha yake ya matendo.

Lakini kama itawezekana, jishughulishe zaidi kuzungumza na watu wengine ili kwa kiasi Fulani huyo mwenzako aweze kuona kuwa hukumpa kipaumbele cha kwanza.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HAPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
 
VITUKO VYA MTAA Copyright © 2016