BOFYA "LIKE" KUUNGANA NASI

Cancel

WAUMINI WA GWAJIMA WAFUNGA SIKU 40 KUMUOMBEA

WAKATI mambo yakiwa bado tete juu ya afya ya kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Mchungaji Josephat Gwajima, wafuasi wake wametangaza kufunga kwa muda wa siku 40 kuanzia juzi Jumatatu ili kuomba.
Mchungaji Josephat Gwajima akiwa hospitali.
Chanzo kilicho ndani ya kanisa hilo ambalo kwa sasa makao makuu yake yapo Kawe, kililiambia gazeti hili kuwa wafuasi hao wameamua kuliacha suala hilo mikononi mwa Mungu, hivyo wameona ni vyema kufunga kwa muda huo ili kumuombea kiongozi wao apate afya njema, lakini pia misukosuko inayomuandama imalizike.
“Jamaa wameona hali sasa inakuwa ngumu, wanafunga kwa vikundi, kila mmoja anamuombea apate afya njema baada ya kuzidiwa wakati akihojiwa, lakini pia wanataka haya mambo yamalizike, kwa hiyo wameona ni bora kumuachia Mwenyezi Mungu ili ayamalize,” kilisema chanzo hicho.
Mmoja wa wachungaji viongozi wa kanisa hilo aliyeulizwa na gazeti hili juu ya jambo hilo, huku akitaka jina lake lihifadhiwe kwa vile siyo msemaji, alikiri waumini kuamua kufunga kwa vikundi, wakiomba katika maeneo yao ili afya na matatizo ya kiongozi wao yaishe haraka.
Waumini.
Mchungaji Gwajima alianguka ghafla wakati akihojiwa na maofisa wa Polisi wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, kufuatia maneno yake ya kashfa dhidi ya Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarb Kardinali Pengo.
Baada ya kuanguka, mchungaji huyo amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni ambako hali yake imeelezwa kuwa bado tete, huku kukiwa na taarifa za kukamatwa kwa watu 15 wanaodaiwa kupanga mipango ya kumtorosha kiongozi huyo wa kiroho kutoka mikononi mwa polisi wanaomlinda.

»

MAMA ANAWA MIKONO UGONJWA WA BANZA

MAMA mzazi wa mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi aliye mgonjwa, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ aitwaye Khadija, amenawa mikono kuhusiana na ugonjwa wa mwanaye, akisema akiwa mzima, alifanya kila aliloweza kumshawishi aache pombe, lakini hakufanikiwa, kwani anaamini maradhi yake pamoja na mambo mengine, yamesababishwa pia na kilevi.
Mwanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’.
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Sinza-Kijiweni, jijini Dar es Salaam, Bi. Khadija alisema hali ya mwanaye hivi sasa bado ni tete, kwani hasikii kiasi cha kufanya mawasiliano kwa tabu na kwamba hata kuinuka kitandani ni shida.
“Mwanangu nilikuwa namwambia kila siku, aachane na ulevi lakini hakutaka kunisikia, ungekuta hayupo kwenye hali hii, huu ni ubishi wake, mimi namwachia Mungu ndiyo aamue maana sina uwezo wa kumfanya anyanyuke kitandani, kikubwa tunachofanya ni kumhudumia tu,” alisema kwa huzuni.
Katika hali nyingine, Banza ni kama aliyechanganyikiwa kwani anachoulizwa sicho anachojibu na hata akiimba wimbo, anamtaja mwimbaji ambaye siyo. Aidha, maneno mengi anayozungumza hivi sasa yanakuwa hayaeleweki.
Wakati mama mzazi akitoa matamshi hayo, wanafamilia wengine walipoulizwa kuhusu mwitikio wa wasanii wenzake kwenda kumjulia hali, wakiwemo aliofanya nao kazi, walisema tangu aanze kuumwa kiasi cha mwezi mmoja uliopita, hakuna msanii aliyewahi kwenda kumjulia hali.
“Unajua kumjulia mtu hali ni moyo wa mtu, hivyo hatuna la kusema zaidi ya kuendelea kumhudumia ndugu yetu,” alisema kaka yake Banza aliyejitambulisha kwa jina la Hamis.
Hii siyo mara ya kwanza kwa msanii huyo kupatwa na maradhi yaliyomlazimisha kulala nyumbani kwa muda mrefu na wadau mbalimbali kwa nyakati tofauti wamekuwa wakihusisha hali hiyo na unywaji pombe wa kupitiliza.
Nyota huyo pia amewahi kuzitumikia kwa mafanikio makubwa Bendi za African Stars ‘Twanga Pepeta’, Tanzania One Theatre (TOT), Extra Bongo na Bambino Sound.

»

BINTI WA MIAKA 23 ADAKWA HOSPITALI YA MWANANYAMA KWA WIZI

MREMBO mmoja aliyejulikana kwa jina la Mariam Moshi (23), mkazi wa Mwananyamala Ujiji, aliponea chupuchupu kuuawa na wagonjwa wenye hasira kali waliolazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar baada ya kudaiwa kuiba nguo.Mariam Moshi akihamaki baada ya kukamatwa na nguo anazodaiwa kuiba katika wodi ya wazazi Hospitalini Mwananyamala.  Walinzi wa hospitali hiyo walimuokoa mrembo huyo kwa kumnasua mikononi mwa wagonjwa hasa wajawazito walioenda kujifungua, waliodai kwamba Mariam aliingia katika wodi yao na kuwaibia.Tukio hilo lilitokea Machi 27, mwaka huu saa tisa alasiri, ambapo mama mmoja ndiye alishtuka kwa kuona amechukuliwa kitenge chake kipya.
Mama huyo alipobaini ameibiwa, alitoka nje na kuangaza macho huku na kule akiangalia alipoelekea Mariam aliyekuwa wodini kwao, ndipo alipomuona akiwa anatoka nje kulielekea geti ambapo aliwapigia kelele walinzi ili wamzuie.
Mariam akiwa mikononi mwa mlinzi wa hospitali hiyo.
“Walinzi walimsimamisha na kumuuliza kama aliiba kitu chochote wodini akirudishe, lakini alikataa katakata kuhusika ma wizi huo,” kilisema chanzo.
Hata hivyo, walinzi walipompekua, aligundulika kuwa na vitu alivyovifunga na kufunika kwa dera (gauni kubwa, refu alilokuwa amevaa).Askari wa kike walipomfunua gauni hilo, walimkuta akiwa na taulo ambalo alikuwa amelifunga kiunoni pamoja na kitenge alichokuwa akituhumiwa kukiiba wodini.
Baada ya wagonjwa kuona mali alizoiba mrembo huyo, ndipo akina mama wengine wakiwa na watoto wao walitoka wodini na kuanza kupiga makelele kwa hasira wakitaka apewe mkong’oto.
Walinzi hao wakitoa baadhi ya vitu alivyoiba.
Hata hivyo, walinzi wa hospitali hiyo walipoona Mariam amezongwa, ilibidi watumie nguvu kumuokoa na kumweka chini ya ulinzi wakisubiri namna ya kumpeleka polisi.Mariam alipohojiwa na waandishi wetu juu ya kitu kilichompeleka hospitalini hapo, alisema alikwenda kuwaona wagonjwa ambao hata hivyo alishindwa kuwataja. Alisema yeye ni mwenyeji wa Dodoma anayeishi Dar kwa kujitegemea.
Aliomba msamaha kwa kitendo alichokifanya, akisema kinatokana na maisha magumu na katika hali ya kushangaza zaidi, alipoulizwa kuhusu taulo alilokuwa amejifunga ndani ya dera alilovaa, alisema halikuwa la hospitalini hapo, bali aliliiba katika gesti aliyokuwa amelala siku hiyo.
...Wakimuhoji.
Wauguzi wa hospitali hiyo walidai malalamiko ya wagonjwa kuibiwa mali zao hospitalini hapo ni jambo la kawaida, hivyo siku hiyo ilikuwa ni ‘40’ ya Mariam.

»

SKENDO WODINI: MAMA ADAI KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME, APEWA WA KIKE TENA MAITI

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kufuatia mwanamke mmoja, Rukia Fikiri (pichani) kudai kujifungua mtoto wa kiume kisha baadaye kukabidhiwa mtoto wa kike akiwa amefariki dunia, Uwazi linatiririka.Tukio hilo la kushangaza lilijiri Machi 25, mwaka huu katika wodi ya wazazi ya hospitali hiyo. 
Rukia Fikiri(kulia) akiwa na ndugu zake wakiwa wamebeba maiti ya mtoto wanaodai kubadilishiwa na manesi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
MSIKIE MWENYEWE
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita hospitalini hapo, Rukia alisema alijifungua mtoto wa kiume mwenye afya njema saa 6 usiku wa Machi 24, mwaka huu na kwamba baada ya kujifungua alionyeshwa kisha aliondolewa leba na kupelekwa Wodi ya Wazazi 7 B.
“Lakini kutokana na uchungu wa uzazi kule wodini nilipitiwa na usingizi. Nilipokuja kuamka, manesi waliokuwa wakinihudumia na mtoto wangu waliniambia mtoto amefariki dunia.“Niliumia sana, nilitoa taarifa kwa ndugu zangu akiwemo mume wangu ambapo walifika hapa tukakabidhiwa maiti huku manesi wakisema wameifunga kwa nguo, wakasema tukaifungulie nyumbani,” alisema Rukia, akaongeza:
“Tulienda nyumbani kwa wakwe zangu eneo la Chamwino. Tulipofungua maiti kwa lengo la kuiosha ili tukaisitiri, tulishangaa kuona ni ya mtoto wa kike badala ya wa kiume.”“Haraka sana tukagundua manesi walitubadilishia. Tulikaa kikao cha dharura cha familia, tukakubaliana tuirudishe maiti hapa. Mimi ninamtaka mtoto wangu wa kiume awe hai au amekufa,” alisema mwanamke huyo huku akiangua kilio kwa uchungu.
 
Rukia Fikiri anayedai kubadilishiwa mtoto huyo.
MUME NAYE AZUNGUMZA
Mume wa Rukia, Hamidu Fikiri naye alipata fursa, akazungumza na Uwazi na kusema:
“Kitendo walichofanya wale manesi ni cha kushangaza sana, kama nisipopewa mwanangu tutaelewana vibaya, mimi nimeshakwenda polisi.”
Mama mzazi wa Hamidu, Mariam Seif ambaye ni bibi wa mtoto alisema kitendo cha mjukuu wake ‘kuibwa’ wodini kimemsikitisha na hawezi kuzika mtoto wa mtu mwingine.“Tulipomrudisha mtoto hapa hospitalini, manesi walikuwa wakitupiana mpira, wale wa wodi 7 B wanasema tatizo liko leba, wa leba wanasema kinyume chake,” alisema bibi huyo.Taarifa zinasema, polisi waliamuru mwili wa mtoto huyo uhifadhiwe hospitalini hapo huku uchunguzi ukiendelea.
Uwazi lilipompigia simu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Rita Lyamuya hakupatikana ofisini kwake na hata alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya mkononi, iliita bila kupokelewa.
 
MASWALI MAGUMU
Ndani ya cheti cha mzazi kulazwa na kuruhusiwa kuna maandishi ya msingi wa uzazi yanayosomeka: Complete Abortion ‘CA’  (mimba kuharibika) ikimaanisha ndicho kiini cha mzazi huyo kufikishwa hospitalini hapo.
Uwazi lilijiuliza kwa nini cheti hicho kiandikwe hivyo wakati mzazi anadai alijifungua salama tena leba?
Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo), alipoulizwa na gazeti hili kuhusu hali hiyo, alisema: “Complete Abortion ni mimba imetoka kabla ya muda wa kujifungua. Lakini kama huyo mama aliingizwa leba ina maana alijifungua, wasingeandika Complete Abortion, wangeandika SB, kwamba amejifungua salama.
“Mwanamke wa CA hawezi kupelekwa leba. Kutakuwa na tatizo katika uandishi wa hicho cheti. Kwani mtoto mwenyewe alikuaje hata kama alifariki dunia?”Uwazi: “Mwili wa mtoto upo kamili, ila ni marehemu tu.”
Dokta: “Sasa CA mtoto hawezi kuwa kamili. Nadhani hapo katika uandishi wa cheti pana tatizo.”

»

TAMKO LA MAASKOFU NA WACHUNGAJI KUTOKA MADHEHEBU MBALIMBALI JUU YA TUKIO LA ASKOFU GWAJIMA.

TAMKO LA MAASKOFU NA WACHUNGAJI KUTOKA MADHEHEBU MBALIMBALI JUU YA TUKIO LA ASKOFU GWAJIMA.
Sisi maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali tumeshtushwa na kusikitishwa kwa taarifa ya ugonjwa wa Askofu na mtumishi mwenzetu Josephat Gwajima ambaye tarehe 27/03/2015 alifika kituo cha polisi cha kati kuitikia wito wa polisi uliomtaka kwenda kujibu shutuma za kutumia lugha ya matusi kwa kardinali Pengo.
Tumepata fursa ya kutafakari na kujadili kwa kina hali iliyompata Askofu mwenzetu hasa baada ya kuzingatia kuea Askofu Gwajima alifika polisi akiwa mzima na mwenye afya njema lakini wakati wa akihojiwa na polisi, hali yake ilibadilika ghafla kiasi cha kupelekea yeye kulazwa hospitali ya TMJ akiugua tena kwenye wodi ya wagonjwa mahututi yaani (ICU) katika chumba cha uangalizi maalum.
Maswali yetu makuu ni kitu gani kimempata mwenzetu? Tunajiuliza, je vyombo vya usalama vimekua sio sehemu salama kama zamani?
Tukiwa bado tunatafakari hill, tumeshtushwa tena baada ya kupata taarifa ya kuwa Wachungaji Wasaidizi wa Askofu Gwajima pamoja na walinzi wake waliokuwepo hospitalini hapo kwa ajili ya kumuuguza nao pia wamekamatwa kwa tuhuma za. kutaka kumtorosha Askofu Gwajima. 
Jambo hili linashangaza zaidi maana wachungaji wale wale waliokuwa naye akiwa mzima wa afya wakati anaelekea polisi ndio wale wale wanatuhumiwa kutaka kumtorosha akiwa mgonjwa.
Ni jambo la kushangaza na lisiloingia akilini kuwa wasaidizi hao wa Gwajima walitaka kumtorosha wakati Gwajima kama angekua na nia hiyo angekwisha fanya hivyo mana alikuwa na uwezo wa kutoroka alipokua Arusha kwenye kikao cha Maaskofu wakuu wa makanisa ya Kipentekoste ambao alipata taarifa za kuitwa Polisi.
Isitoshe Gwajima aliitija wito na kwenda polisi mwenyewe kwa miguu yake bila kushurutishwa, wala hakufikishwa polisi kwa nguvu.
Swali: Kama alikua anaona ugumu wa kutoroka wakati hakuna polisi anayemlinda na huku akiwa mwenye afya tele, itakuaje rahisi kutoroshwa leo akiwa mahututi na akiwa kwenye ulinzi mkali wa polisi?
Mbona hii inastaajabisha?
Jambo jingine linalotupa shida ni kuhusu mlalamikaji wa kesi hii inayomkabili Askofu Gwajima. Tumeelezwa na wasaidizi wa Askofu Gwajima kuwa pale polisi walielezwa kuwa aliyefungua kesi hii sio Pengo ila mtu mmoja aitwaye Aboubakar.
Kwa ufahamu wetu juu ya sheria unatutuma kuamini kuwa Aboubakar sio MTU sahihi wa kufungua kesi hiyo sababu hawezi kutuonyesha ameumizwa kiasi gani na matamshi ya Askofu Gwajima.
Isitoshe, Kardinali Pengo mwenyewe ametamka katika Ibada yake ya Jumapili hii ya tarehe 29/03/2015 kuwa amemsamehe Gwajima, yupi tena mwenye uchungu wa kumzidi Kardinali Pengo?
RAI YETU:
Rai yetu ni kwamba, ni vizuri serikali pamoja na vyombo vyake vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi wake kwani yanaweza kusababisha chuki dhidi ya serikali na pia kupelekea mpasuko mkubwa wa kidini katika jamii yetu iliyo na historia nzuri ya umoja na mshikamano na ushirikiano katika matukio yote ya kimaisha.
Tunaomba serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu na busara kubwa itumike ili kuepusha uvunjifu wa Amani katika jamii.
MAAMUZI YETU:
Jambo hili linazungumzika, maana hata hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili kupata suluhisho juu ya jambo hili.
Kwa niaba ya maaskofu na wachungaji:
Mwenyekiti: Askofu Dr. Mgullu Kilimba
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa
Na mwandishi
F.A.K
30/03/2015

»

MSICHANA MTANZANIA AKAMATWA KWA UGAIDI KENYA, ALIKUWA ANAENDA KWENYE MAFUNZO YA KUJITOA MHANGA SOMALIA

Vyombo vya usalama nchini Kenya, vinawashikilia wasichana watatu akiwamo Mtanzania, kwa kile kunachodaiwa kutaka kujiunga na kundi la kigaidi la al-Shabaab huko Somalia.
Taarifa kutoka kwa Kamishna wa Polisi Jimbo la El -Wak, mpakani mwa Kenya na Somalia, Nelson Marwa amesema Mtanzania aliyekamatwa, alijieleza kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika, Sudan.

Mtanzania huyo, Ummul-Khayr Sadir Abdul (19), mwenyeji wa Zanzibar, anatajwa kuwa kiongozi wa kundi hilo lililopanga kujiunga na al-Shabaab.
Wasichana wengine waliokamatwa pamoja na Ummul-Khayr, ni Maryam Said Aboud na Khadija Abubakar Abdulkadir wote raia wa Kenya.

“Hawa wasichana watatu, inaaminika kuwa walikuwa wanakwenda Somalia kupata mafunzo ya kigaidi na baadaye kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga,” alisema Kamishna Marwa.
Akizungumzia suala hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Diwani Athumani alisema: “Tunafuatilia hatujapokea taarifa zaidi ya hizo.”
Kamishna Marwa alisema raia hao wawili wa Kenya, mmoja ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya kilichopo Thika, Jimbo Kiambu na mwingine ni mwanafunzi wa Sekondari ya Burhania, iliyopo Malindi, Kilifi.

“Serikali imepata taarifa kuhusu watu wanaokusanya watu kutoka Afrika Mashariki ili wakajiunge na makundi ya ugaidi nchini Somalia, wakala wetu wa usalama wamepata taarifa hizo na kufanikisha kukamatwa kwa wasichana hao,” alisema Kamishana Marwa.
Hivi karibuni, tovuti ya al-Jazeera ilitoa taarifa za kukamatwa kwa mkanda wa video ulioonyesha mwakilishi wa kundi la kigaidi la Dola ya Kiislamu ya Iraq na Levant (ISIL) akimtaka kiongozi wa kundi la al-Shabaab kuliimarisha kwa kufanya mashambulizi ya kigaidi katika miji ya Mwanza na Dar es Salaam.

Kamishna Marwa alisema ingawa nyaraka za wasichana hao zote zinaonyesha kuwa ni wanafunzi, lakini bado walibanwa kwa maswali kuhusu sababu inayowapeleka nchini Somalia.
Aliongeza zaidi kuwa chanzo cha habari cha kiusalama kilieleza kuwa nyaraka za wasichana hao zilionyesha kuwa walikuwa wakienda kuolewa na wanajeshi wa kundi la al-Shabaab.

»

MBUNGE SHYROSE BHANJI AFUNGUKA UGONJWA UNAOMSUMBUA

Mbunge katika bunge la Afrika Mashariki,Shyrose Bhanji amefunguka ugonjwa unaomsumbua kwa muda mrefu uliomfanya alazwe katika hospitali ya Agha Khan,jijini Dar.

Akizungumza na Clouds Fm, Shyrose alisema kuwa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Pumu(asthma) kwa muda mrefu tangu akiwa mdogo lakini safari hii ugonjwa ulizidi sana hali iliomfanya kulazwa hospitali kwa siku kadhaa.

"Huu ugonjwa huwa unanisumbua kwa muda mrefu lakini hadi kufikia hatua ya kulazwa ni safari hii hali ilikuwa mbaya sana lakini namshukuru Mungu nimepewa matibabu naendelea vizuri,’’alisema Shyrose.

Aidha aliongeza kuwa mara ya mwisho kuugua hadi kufikia hatua ya kulazwa ilikuwa miaka mingi sana wakati akisoma nchini Uingereza,pia hali ya hewa ya baridi huwa ni tatizo kwake.

»

MWANAMUZIKI SUMA LEE AKATA SHAURI AAMUA KUACHA MZIKI, AAGIZA NYIMBO ZAKE ZIFUTWE NA REDIO WASIZIPIGE TENA

Hit maker wa ‘Hakunaga’, Suma Lee amesema kuwa hatafanya tena muziki kwasababu ameachana kabisa na maisha hayo na ameamua kusomea dini ya kiislam

Suma ambaye alitengeneza pesa nyingi kupitia hit yake ya ‘Hakunaga’, amesema kuwa hana mpango wa kuzitoa nyimbo zake zilizoko studio ambazo hazijatoka.

“sifanyi tena muziki na nimeachana kabisa na maisha hayo, na nyimbo zote zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke baada ya kuzilipia, “ Alisema Suma.

“kuna wimbo mmoja nimefanya na Cp ambao ndio ulikuwa wa kurudisha kundi la Parklane, pia nimeuzuia, labda Cp auchukue yeye.Kilichobaki ni kuwaombea wazazi wetu waliotutangulia, wengine walikuwa hawataki tufanye kazi hizi, kwa kuwa hawapo na hakuna wakutukataza tena, bora tukae na kuwaombea.”

»

GWAJIMA AFUNGUKA:ASEMA ALIAGIZA BASTOLA YAKE ILI AJIHAMI BAADA YA TAARIFA KUZAGAA MITANDAONI KUWA AMEFARIKI DUNIA

Hii  ni  Picha  iliyosambazwa  katika  mitandao  ya  kijamii  ikidai  kuwa  Gwajima  kafariki  dunia  na  yuko  Mochwari.Taarifa  hizi  zilimpa  hofu  Gwajima  na  kumfanya  Aagize  Bastola  yake  kwa  ajili  ya  kujihami.
**********

Utata umeibuka kuhusu bastola waliyodaiwa kukamatwa nayo wafuasi wa Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima baada ya kiongozi huyo kusema anaimiliki kihalali kinyume na maelezo ya polisi.
  
Gwajima aliyetolewa kwenye chumba cha uangalizi maalumu cha Hospitali ya TMJ jana, amelitaka Jeshi la Polisi kurudisha bastola hiyo, akisema ni mali yake na aliiagiza ipelekwe hospitalini kwa sababu ya kujilinda.
 
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo alipolazwa baada ya kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu akiwa katika mahojiano na polisi, Gwajima alisema anashangaa kukamatwa kwa wachungaji wake waliokuwapo kwa ajili ya kumlinda.
 
Hata hivyo, katika kwa upande mwingine, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema bunduki hiyo haina umiliki halali wa Gwajima wala wa wachungaji 15 waliokamatwa lakini baadaye jioni baada ya maelezo ya Gwajima, alitoa taarifa akisema bastola hiyo ni mali halali ya askofu huyo. Pia alisema kuhusu risasi 17 za bunduki aina ya Shortgun, Gwajima anamiliki bunduki ya aina hiyo lakini akasema uchunguzi kuhusu watu hao 15 unaendelea.

Kauli ya Gwajima
Akizungumza kwa shida akiwa amejishika tumbo, Gwajima alisemaalipopata taarifa za uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia, aliagiza wachungaji waende hospitalini kwa ajili ya kumlinda, lakini wakaishia mikononi mwa polisi wakidaiwa kutaka kumtorosha.
 
Alisema alihofia kuwapo kwa watu wabaya ambao wangeweza kumdhuru halafu wakasingizia kitendo hicho kufanywa na polisi kwa kuwa alipata tatizo akiwa mikononi mwao.
 
“Usiku wasiwasi ulizidi, huku kila mmoja akiwa hafahamu kwa nini ujumbe wa namna ile unasambazwa kwenye mitandao, msambazaji ni nani, ana nia gani, nikaamua kuwaagiza waniletee silaha yangu iliyokuwa kwenye begi ili likitokea lolote niweze kujilinda,” alisema Gwajima.
 
Alisema alishangaa kukamatwa wachungaji wake na kuchukua silaha iliyokuwa ndani ya begi na hadi jana hakuwa ameulizwa chochote kuhusu umiliki wa silaha hiyo.
 
“Kabla sijazungumza na waandishi kueleza ukweli wa kinachodaiwa kuwa nilitaka kutoroshwa na wachungaji wangu, nilitaka kuzungumza na ZCO (Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu), lakini hajaja, kadi ya ile silaha ninayo,” alisema Gwajima.
 
Alisema madai kuwa alitaka kutoroka ilihali polisi alikwenda mwenyewe akitokea Arusha baada ya kusoma katika vyombo vya habari kuwa anatafutwa.
 
Alifafanua kuwa hata alipofika polisi kwa ajili ya mahojiano hakuwa na shaka hata kidogo, lakini alishangaa kuona anaishiwa nguvu kila baada ya muda na alipoona kichwa kinamuuma, akawaomba wampeleke hospitali ili mambo mengine yafuate baadaye, kitu ambacho hakikufanyika kwa wakati.
 
Wasiwasi kwa polisi
Alisema alijaribu kuomba apelekwe hospitali mara kadhaa, lakini hakuna aliyekubaliana naye hadi alipopoteza fahamu na kupelekwa hospitali ya Polisi Kurasini.
 
“Hivi hata kama ni chombo cha usalama, nimepata matatizo nipo mikononi mwao, halafu nikubali kutibiwa katika hospitali yao, sikulitaka hilo na hata waliposema nikatibiwe Muhimbili pia sikutaka, ndiyo maana nilikuja hapa, sisemi moja kwa moja kama Polisi wanahusika lakini kuna vitu vinanitia shaka,” alisema Gwajima.
 
Alieleza kuwa anatilia shaka Jeshi la Polisi kutokana na kuwapo vitu vingi vinavyoashiria wana kitu kingine wanatafuta, kwani jana tulikuwa na hofu ya kuvamiwa, waliokuja kutuvamia ni wao, sikugombana na Pengo, nilikuwa namkemea kama kiongozi mwenzangu wa kiroho wao, wameligeuza ni kesi.
 
“Sijawahi kulitilia shaka Jeshi la Polisi lakini katika hili napata wasiwasi mwingi, sina ugomvi na Kardinali Pengo, nampenda, hajanilaumu, wala kunishtaki, nilikuwa namkemea katika masuala yetu ya mabaraza ya dini na siyo vinginevyo,” alisema Gwajima.
 
Gwajima pia alionyesha wasiwasi wake kwa kile kilichokuwa kinang’ang’aniwa na polisi kwenda kupekua nyumbani kwake kuwa hakikuwa kitu kizuri.
 
Kova alipinga
Wakati Gwajima akisema hayo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema bastola waliyokutwa nayo wafuasi wa Gwajima haimilikiwi kihalali.
 
“Tumegundua kuwa katika wale watu waliokuwa pale akiwamo Gwajima mwenyewe, (bastola) haikuwa  katika umiliki wao halali, kwa hiyo hapa kuna kesi ya kupatikana na silaha bila kibali.”
 
Akizungumzia tuhuma kwamba polisi walimpekua mke wa Gwajima, Kova alisema hakuna polisi waliofika nyumbani kwake kufanya upekuzi wowote na kama wakitaka kufanya hivyo watafuata taratibu maalumu za upekuzi.
 
Akijibu swali kuhusu mahali Gwajima alipotakiwa kutoroshewa, Kova alisema uchunguzi huo bado unaendelea na utakapomalizika wahusika watafikishwa mahakamani.
 
Pia alipoulizwa kama Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amemsamehe Gwajima, kwani polisi imng’ang’anie, Kova alisema;“amesema anamsamehe lakini haingilii mambo ya sheria.”
 
Kuhusu sababu za Gwajima kuzimia wakati akihojiwa, Kova alisema anayepaswa kuulizwa kwa nini alianguka wakati akihojiwa na polisi ni Gwajima mwenyewe.
 
“Siri za mahojiano huwa hazitolewi kabla ya ushahidi mahakamani, sababu ya kupata shock (mshtuko) atajua mwenyewe, kwa kuwa ukifanyiwa jambo ukafurahi au ukachukia wewe ndiyo unajua ilikuwaje, chochote kitakachotokea ukicheka, ukinuna, ukizimia, wewe ndiyo tukuulize ilikuwaje mpaka ukazimia kwa sababu hisia unazipata wewe,”alisema Kova.

Makonda amtembelea
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye alikuwa amemwandikia Gwajima barua akimwita ofisi kwake, jana mchana alimtembelea hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali kiongozi huyo lakini akasisitiza kuwa nia yake bado ipo palepale.
 
“Nilimtaka leo aripoti ofisini kwangu lakini kwa bahati mbaya anaugua na amelazwa. Nitakwenda kumuona ili nijue hali yake ikoje,” alisema Makonda kabla ya kufunga safari kwenda hospitali alikolazwa.
 
Alisema pia atataka kiongozi huyo wa kiroho amweleze anavyoelewa maana ya uhuru wa kuabudu unaoelezwa katika Katiba, usajili wa taasisi yake na katiba ya taasisi hiyo. 
  
“Mimi ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Niliagiza polisi wamkamate na baadaye wakimaliza kumhoji aje kwangu pia atahojiwa na jopo la watu 20,” alisema Makonda.

»

AIBU:MZEE MAJUTO ADAIWA KUZAMA KWENYE PENZI LA MJUKUU WAKE

Komediani kipenzi cha wengi Bongo, Majuto Athuman ‘Mzee Majuto’, anadaiwa kuzama kwa mara nyingine kwenye penzi la msichana mbichi anayekadiriwa kuwa na umri sawa na mjuu wake.
Komediani kipenzi cha wengi Bongo, Majuto Athuman ‘Mzee Majuto’.
TUJIUNGE NA MKE WA MZEE MAJUTO
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, mke wa Mzee Majuto aitwaye Aisha Yusuf alikiri kuwa mumewe amenasa kwa ‘kibinti’ chenye umri wa miaka 18.
Aisha alidai kwamba, Mzee Majuto anaishi na binti huyo kama mke na mume, jambo ambalo watu wamekuwa wakimshangaa na kuhoji kwa nini anatoka na mtoto mdogo kiasi hicho wakati ana watoto wakubwa wenye uwezo wa kuzaa msichana kama huyo na akawa mjukuu wake.

MZEE MAJUTO NI KIOO CHA JAMII
“Kinachonichosha mimi kwa nini anafanya hivyo wakati yeye ni kioo cha jamii?
“Watu wengi wanatakiwa kujifunza mengi kupitia kwake, maana tangu aoe hata sisi hatujafurahishwa na jambo hilo ingawa kweli ni uamuzi wake.
“Kingine amekuwa hakai tena hapa nyumbani (Tanga) na kuna kipindi unapita hata mwezi tunawasilia kwenye simu tu labda mtoto aumwe ndiyo atapita tu na siyo kukaa.

NI MJUKUU WAKE KABISA
“Sijui mzee wangu anafanya hivyo kwa nini maana sasa ana zaidi ya miaka 60 na kama mtoto mimi sasa hivi nina umri wa miaka 35 kwake bado mimi mdogo sana na nina umri wa watoto wake wa kuzaa sasa huyo aliyemuoa si ni mjukuu wake kabisa?
“Mimi naona aibu tu kama familia ingawa dini kweli inaruhusu lakini si kwa mtoto kama yule,” alisema Aisha kwa uchungu.

MZEE MAJUTO ANASEMAJE?
Baada ya kumsikia mkewe, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Mzee Majuto ili azungumzie ishu hiyo ambapo simu yake ilipokelewa na msichana mwenye sauti nyororo huku akidai kwamba mzee Majuto amelala apigiwe baadaye.
“Mimi ni mke wake mdogo, Mzee Majuto amelala, nafikiri jaribu kupiga baadaye anaweza kuwa ameamka na utaweza kuzungumza naye vizuri,” alisema.
Mzee Majuto alipotafutwa baadaye, simu yake iliita bila kupokelewa.

WASANII WENZAKE WAMLAANI
Baadhi ya wasanii waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina yao walilaani kitendo cha Mzee Majuto kuwa na binti huyo kwani umri wake umeenda.

»

AUKIMIWA MIAKA 3 JELA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 3

Katika hali ya kushangaza, Wilson Saimon ‘Babu Nyemeni’ (21), mkazi wa Kijiji cha Mgeta wilayani Mvomero mkoani Morogoro yamemkuta baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kudaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.
Wilson Saimon ‘Babu Nyemeni’ (21), mkazi wa Kijiji cha Mgeta wilayani Mvomero mkoani Morogoro aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kudaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.
Babu Nyemeni anadaiwa kufanya unyama huo mwishoni mwa mwaka jana, nyumbani kwa Angel Bosco ambaye alikuwa amekwenda kuimba kwaya kanisani na kumuacha nyumbani mtoto huyo (jina tunalihifadhi) akiwa na mfanyakazi wake wa ndani.
Wilson Saimon akiwa mikononi mwa Polisi.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro, Hakimu Mkazi, Regina Futakamba alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo ambaye ni jirani yake Angel, alimuomba mtoto huyo kwa mfanyakazi wa ndani na kumwambia anakwenda kumnunulia pipi, mfanyakazi alimkubalia ndipo alipokwenda kumbaka kichakani, jambo ambalo mtuhumiwa huyo alilikiri mahakamani.
Alisema mtoto huyo alikutwa katika kichaka kilicho nje kidogo ya kijiji hicho akiwa analia kwa maumivu ndipo walipompeleka kwenye Zahanati ya Mgeta alikobainika alibakwa na kuharibiwa sehemu za siri.
Mama wa mtoto aliyebakwa.
Hakimu Regina alisema kutokana na kosa hilo, mtuhumiwa alitakiwa kufungwa kifungo cha maisha lakini alitoa nafasi kwa mtuhumiwa kujitetea ambapo alijitetea na hakimu kumpunguzia adhabu hiyo kwa kumfunga miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa wengine.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wananchi wa Mgeta walilihusishwa tukio hilo na imani za kishirikina kwani walisema walishangazwa na mtuhumiwa kumbaka mtoto mdogo kiasi hicho.
“Mh! Hii nahisi inawezekana kadanganywa na waganga kwamba atembee na mtoto mdogo ndiyo apate utajiri maana haya mambo nayo yapo,” alisema mkazi mmoja wa Kijiji cha Mgeta

»

VURUGU NA MATUSI ZATAWALA KWENYE SEMINA YA WABUNGE KUHUSU SAKATA LA MAHAKAMA YA KADHI......WABUNGE WEGI WAPINGA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA HIYO

Mambo magumu yameibuka katika suala la kujadili uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, baada ya kutokea  malumbano makali na vurugu huku idadi kubwa ya wabunge wakiitaka serikali kuuondoa Muswada wa Mahakama ya Kadhi usiwasilishwe bungeni.
Wabunge wengi walisema kufanya hivyo kunaweza kusababisha mpasuko na kuvunjika kwa amani nchini.
Aidha, wamesema suala la Mahakama ya Kadhi linataka kufanywa kama mtaji wa kisiasa kwa baadhi ya viongozi wanaotaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu ili kutafuta kura za Waislamu.
Mvutano huo uliibuka jana wakati wa semina ya wabunge kujadili Muswada wa Sheria mbalimbali wa mwaka 2014 ambao ndani yake kuna  Muswada wa Mahakama ya Kadhi ambao umepangwa kuwasilishwa Aprili Mosi mwaka huu siku ya kuahirisha mkutano wa 19 wa Bunge.
Mbunge wa Ngara (CCM), Deogratias Ntukamazina, alisema Kamati ya Katiba Sheria na Utawala ilipowaita viongozi mbalimbali wa dini kuzungumzia suala hilo Waislamu walitofautiana katika suala la uteuzi wa Kadhi kufanywa na Mufti Mkuu wa Tanzania na wakataka waelewane kwanza kabla ya suala hilo kupelekwa bungeni.
Alisema katika mkutano huo makundi 11 ambayo hayakubaliana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), walisema Muswada wa Mahakama ya Kadhi uletwe bungeni baada ya kuridhiana kwa sababu hawakubaliani na Bakwata ambalo kiongozi wake ni Mufti Mkuu wa Tanzania.
Walisema maaskofu walisema hawana tatizo na suala la Mahakama ya Kadhi, lakini isiwe na muundo kama wa mahakama nyingine na kwamba mawazo ya waasisi wa Taifa, hawakutaka serikali iwe na dini na ndiyo maana hawakuruhusu mahakama hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Rukia Kassimu, alihoji ni kwanini Mahakama ya Kadhi inataka kuundwa na kupewa jukumu Mufti ambaye anatoka Bakwata ambayo ni taasisi binafsi na imesajiliwa na Mamlaka ya Rita.
“Bakwata ni taasisi kama zilivyo taasisi nyingine, haikubaliki, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliahidi suala la Mahakama ya Kadhi ili Waislamu wampigie kura kwa sababu anataka kugombea urais mwaka huu, alisema.
Rukia alisema ni marufuku serikali kuwalazimisha Waislamu kuwa chini ya Bakwata na kwamba Waziri Mkuu, Pinda anafahamu kwa kina suluhisho na mvutano huo wa Mahakama ya Kadhi.
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR), Moses Machali,  alisema suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na kuingizwa katika mfumo wa mahakama za kawaida inajichanganya na ibara ya 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema mwaka 2011 Rais Jakaya Kikwete wakati anazindua msikiti wa Gadaf alisema suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi lisihusishwe na serikali kwa sababu wapo watu wengine ambao kila mmoja ana imani yake.
Alisema hatua ya serikali kutaka kuuleta muswada huo wakati bado Waislamu wenyewe hawaelewani ni kuwakosea Waislamu na kwamba inawezekana Waziri alilizungumzia suala hili sababu ya malengo yake ya urais.
Machali alisema kama muswada huu utapelekwa Bungeni itatoa fursa kwa madhehebu mbalimbali kila moja kuanzisha mahakama yake hali itakayoleta machafuko nchini kwa kuwa nchi itakuwa katika mfumo wa mahakama za dini.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema muswada unapendekeza kutambua kitu ambacho mfumo wa sheria za nchi hauna na kwamba uongo unaotumiwa na serikali ndiyo unafanya watu wawe na hofu.
Mbunge wa Nkasi Kusini (CCM), Ally Kessy, alisema: “Katika nguzo tano za Kiislamu Mahakama ya Kadhi haipo, nguzo sita za imani pia haipo, sasa inakuwaje wanadai kitu ambacho hakitambuliki katika nguzo za kiislamu.”
Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa, alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi urudishwe ukaboreshwe badala ya kuharakisha kuupeleka bungeni wakati bado una utata hata kwa waislamu wenyewe.
Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambali Nyangwine, alisema Muswada  wa  Mahakama  ya  Kadhi usimamishwe ukafanyiwe utafiti kwanza kwa sababu ndani ya Waislamu wenyewe hawaelewani.
Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, alisema Wabunge wasipokuwa makini na suala la Mahakama ya Kadhi, Bunge litaingia katika historia kuvunjika kwa amani.
Selasini alisema serikali iachane na kutoa ‘jini’ lililofungiwa na waasisi Mwalimu Nyerere na Karume na kwamba tukifanya mchezo nchi itabaki katika vipande vipande.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Mary Mwanjelwa,  alisema jambo hili litaligawa Taifa na kwamba waasisi hawakuwa wajinga walipokataa serikali isiwe na dini.
Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa, alisema nchi inaelekea kubaya kwani msingi wa kuleta Mahakama ya Kadhi ni kutaka kuwachota Waislamu kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
“Serikali kama imedhamiria kuleta Mahakama ya Kadhi ilete katika utaratibu mzuri, lakini kwa huu utaratibu ni unafiki na mwenyezi Mungu hapendi unafiki, tusiwahadae Waislamu,” alisema.
 Khalifa alisema kwa hali ilivyo muswada huo haujaiva na kwamba usiletwe  bungeni hadi hapo serikali itakapojipanga vizuri.
 Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema),David Silinde, alisema suala la imani siyo la chama cha kisiasa kwani suala la Mahakama ya Kadhi litaipeleka nchi kubaya na inawezekana ikawa ndio mwisho wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Mnataka kutuvurugia nchi sababu ya kutafuta kura za Waislamu, kwa hili Waziri Mkuu umechemka sana, nalisema hili kwa sababu wewe Waziri Mkuu ndiye uliyeahidi kuleta bungeni Muswada wa Mahakama ya Kadhi,” alisema.
Mbunge wa Kisarawe (CCM), Suleiman Jafo, alisema yasifanyike masikhala mswaada huyo uwasilishwe bungeni.
Mbunge wa Mbeya Vijijini (CCM),Mchungaji Lackison Mwanjale, alisema serikali ikajipange upya katika suala la Mahakama ya Kadhi kabla ya kuuleta bungeni muswada kwani bado suala hilo halieleweki kwa jamii.
Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM),Martaza Mangungu, alisema hakubaliani na suala la Mufti kupewa jukumu la kuchagua Kadhi Mkuu wakati Waislamu wengi hawakubaliani na Bakwata ambayo inaongozwa na Mufti.
Mbunge wa Lupa (CCM), Victor Mwambalaswa, alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi wapelekewe wahusika kabla ya kuletwa bungeni ili wajadiliane na kukubaliana mambo ya msingi wanayoona yatawafaa katika uanzishwaji wa mahakama hayo.
 Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Peter Kafumu, alisema serikali imeshindwa kusimamia vizuri suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa kushindwa kuwaelimisha wananchi jambo hilo.
Mbunge wa Chwaka (CCM), Yahaya Kassim Issa, alisema  Waislamu wanataka Mahakama hiyo kwa kuwa wanakosa haki hivyo serikali iruhusu kuanzishwa kwake.
Pinda: Tutatafakari  Upya
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akihitimisha mjadala huo alisema kulingana na maoni yaliyotolewa na Wabunge ameelewa kwamba bado hakuna maelewano miongoni mwa Waislamu wenyewe na pia hakuna uelewa wa jamii kuhusu suala hilo.
Alisema mambo yaliyowasilishwa kuhusiana na muswada huo ni maamuzi ya Bunge Maalum la Katiba na siyo yake, bali anabebeshwa msalaba tu kwa sababu alikuwa anaiwakilisha serikali.
Pinda alisema kutokana na hali hiyo, serikali itakaa kushauriana tena na Spika pamoja na Rais waone wafanye nini katika jambo hilo.
Vijembe  na  Matusi
Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, wakati akichangia hoja hiyo alishindwa kuvumulia baada ya baadhi ya wabunge kuingilia mchango wake kwa kumzomea na kusema maneno yaliyomuudhi na kuamua kuwatolewa maneno ya kuudhi (matusi).
Mbunge wa Fuoni (CCM), Said Mussa Zubeir, aliwaita baadhi ya wabunge walikuwa wakimzomea wakati akizungumza kuwa ni ‘wapumbavu’.
Wakati wa majadiliano hayo ilipofika saa 8:17 wakati Mbunge wa Kisarawe, Jafo akiendelea kuchangia kulitokea vurugu ambazo nusura wabunge wapigane huku baadhi yao wakiamua kutoka ukumbini.
Kutokana na kutokuwapo hali ya utulivu ukumbini, baadhi ya askari pamoja na maofisa usalama waliokuwapo nje, walilazimika kuingia ndani kuhakikisha amani haivunjiki.
Spika wa Bunge, Anna Makinda, alituliza  vurugu  ukumbini kwa kuwataka wabunge wawe wavumilivu wakati wenzao wakichangia.
Katika majadiliano wabunge zaidi 30 walichangia na zaidi ya 20 walikataa muswada wa Mahakama ya Kadhi usiwasilishwe Bungeni  siku ya Jumatano wiki hii.
Kabla ya kuanza majadiliano, Mbunge wa  Kuteuliwa, James Mbatia, alitoa hoja kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja, kwamba wakati wa majadiliano waandishi wa habari wasiwepo ukumbini kwa kile alichoeleza ni unyeti wa jambo hilo.
Hata hivyo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini,Kessy, alisema kama waandishi wataondolewa ukumbini naye atalazimika kuondoka huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, akisema hakuna sababu ya kuwaondoa waandishi kwa sababu jambo linalojadiliwa wananchi wanataka kulifahamu kupitia vyombo vya habari.

»

TEAM WEMA WAKWERA NA TABIA YA WATU KUMZUSHIA WEMA

Baada ya Picha za staa mrembo kutoka Bongo Movies, Wema Sepetu akiwa na mshindi wa Big Brother Africa (BBA) 2014, Idris Sultan wakiwa kwenye moja ya supermarket hapa jijini Dar kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii zaidi ya moto wa vifuu  huku kila mtu akiandika lake kuhusiana na kile alichokiaona, Team Wema waneoneshwa kukerwa na tabia za watu kumzushia Wema  kwenye mahusiano.

Licha ya ukweli ni kwamba Wema na Idris wanaonekana kikazi zaidi, yaani ulikuwa ni wito maarumu kutoka kwa wenye  supermaket hiyo, watu wengi wameolionekana kupakaza kuwa wawili hao ni Le Project mpya na wengi wakimtupia maneno Wema kuwa hisaa amezidiii na wengine wakimlaumu Idris kuwa ameingia chaka.

Kitendi hiki cha Wema kuzushiwa kuwa na mahusiano na watu ambao anafanyanao kazi kimewakera sana Team Wema na kusababisha timbwili la maneno mitandaoni.

Imekua kama tabia ya watu ku comment ( yani ndo umeamua kua na wema) ( wema ndo unatoka na huyu) kwa kila mtu anae fanya nae kazi.. Naomba kuwauliza inamana nyie hamuon kama hizo ni kazi?? Mme shindwa tu kwa Millard Ayo na project ya the completePackage kusema anatoka na wema . Watu wameshindwa kutofautisha kati ya X na + ntaomba Diamond awasaidie kuwapa darasa ama ASEME NA NYIYI. Ama nene".

»

ZITTO AICHOKOZA CHADEMA NA KUWAPA SOMO WANACHAMA WAKE

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT – Wazalendo, Kabwe Zitto ameahidi chama chake kuendesha shughuli zake kwa uwazi, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku viongozi kufanya biashara na chama hicho, jambo ambalo limekuwa likidaiwa kufanyika ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Ndani ya Chadema, mara kadhaa imekuwa ikidaiwa kwamba Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, amekuwa akifanya biashara na chama chake.

Akizungumza wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa ACT-Wazalendo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Zitto, bila kutaja chama wala jina la mwanasiasa yeyote, alisema chama chake kinapozungumzia wananchi kurejesha taifa mikononi mwao ieleweke kwamba wanazungumzia uwajibikaji.

“Chama cha ACT Wazalendo kimeelekeza kikanuni kwamba kila kiongozi wa chama lazima atangaze mali zake na madeni yake. Kila kiongozi lazima aweke wazi maslahi yake ya kibiashara na mengineyo wazi ili kila anapotenda au kusema jambo wananchi wajue maslahi aliyonayo au la katika suala husika.

“Viongozi wote wa kitaifa wa ACT Wazalendo wamefanya hivyo na tutaweka saini zetu mbele yenu kama mashahidi. Naomba Mwanasheria wetu aje hapa tutekeleze matakwa haya ya kikanuni.

“Fomu hizi zitakuwa kwenye tovuti ya chama ndani ya muda mfupi ujao ili kila mtanzaina aone. Kila Kiongozi wa Chama ambaye miiko ya uongozi inamtaja anapaswa kuwa amejaza fomu hizi na kuziwasilisha kwa Katibu wa Kamati ya Uadilifu katika ifikapo tarehe 30 Juni 2015.

“Tunapopinga viongozi wa umma kufanya biashara na serikali na hivyo kuwa na mgongano wa kimaslahi na kushamiri kwa ufisadi, hivyo hivyo tunapinga viongozi wa chama chetu kufanya biashara na chama. Ni marufuku serikali kugeuzwa kuwa genge la watu wachache wanaopora rasilimali za umma. Uadilifu tunaoutaka serikalini ni lazima uanzie kwetu tunaohubiri.

“Tutafanya haya kwa kubadilisha siasa zetu kuelekea kwenye masuala yanayowahusu wananchi; wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara ndogo ndogo, vijana, wanawake na wazee wetu.

“Tunataka kurejesha nchi yetu Tanzania kwa kujenga uchumi wa wote. Tunaporejea kwenye Azimio, hatusemi tunakwenda kutaifisha kila kitu na Serikali kuendesha shughuli zote za kiuchumi. Tunaheshimu na kuthamini sekta binafsi na mchango wake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo.

“Tunamaanisha kuwa ni lazima Dola isimamie uchumi. Sio kazi ya Serikali kufanya biashara. Lakini tunamaanisha kuwa ni lazima kurekebisha baadhi ya makosa yaliyofanyika kwenye ubinafsishaji na hususan ubinafsishaji holela uliofanyika kwenye sekta ya Kilimo na kupora ardhi ya wananchi wetu na kuwageuza kuwa manamba kwenye ardhi yao wenyewe. Tunataka kutomokeza ukwepaji kodi,” alisema Zitto.

CHANZO: Raia Mwema

»

KAKAKE GWAJIMA AMTAKA AMUOMBE RADHI PENGO

Kada wa Chama Cha Mapinduzi , Methusela Gwajima.
Methusela Gwajima (kushoto) akitoa tamko, Pius Yalula (kulia) Afisa habari idara ya Maelezo.
Wanahabri wakifuatilia tukio hilo.
KAKA wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima aitwaye Methusela Gwajima amemtaka mdogo wake kwenda kumuomba radhi Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo kwa kutoa lugha ya kumkashifu.
Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Methusela alisema ameamua kutokufumbia macho kitendo cha ndugu yake kumkashifu Pengo na kwamba anapaswa kujitathimini alipopotoka kwa kumtukana kiongozi mkubwa wa kiroho kwani ni sawa na kuidhalilisha familia nzima ya Ukoo wa Gwajima.
Alisema maneno yake ya kashfa ni dhahili ya kuwa hata ukoo mzima umedhalilishwa hivyo familia ya Methusela Gwajima  imemtaka  kuomba radhi mara moja.
Hata hivyo alisema kuwa yeye ni kada wa CCM hivyo amepata usumbufu mkubwa tokea sakata hilo liibuke maana ndugu na marafiki walioko nje ya nchi wamekuwa wakimuuliza kuhusiana na suala hilo hali inayompa wakati mgumu kuwapatia majibu.
Alisema kashfa hizo hazina tija kwa taifa na haileti uhusiano mwema baina ya madhehebu ya dini, bali  yanachochea  chuki, uhasama, utengano na hasira kati ya wakristo kwa wakristo.

»

BODABODA WAPEWA KICHAPO CHA MBWA MWIZI KUTOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUKWAPUA MKOBA


Mmoja kati ya vibaka hao akiwa hoi baada ya kupata kichapo kikali.

Vijana wawili wa bodaboda ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja, hivi karibuni walikoswakoswa kuuawa baada ya kupora mkoba uliokuwa na simu ya mwanamke aliyekuwa akipita njia.

Tukio hilo lilijiri Jumanne iliyopita, saa 1.30 usiku maeneo ya Sinza Afrikasana, pembeni mwa Baa ya Hongera ambapo inadaiwa ni eneo hatari kwa wizi huo.Shuhuda wa tukio hilo alilitonya gazeti hili kuwa, imekuwa ni tabia kwa baadhi ya vijana kutumia usafiri wa bodaboda kupora watu simu na mikoba hasa wanawake na kwamba siku hiyo arobaini ya vijana hao ilikuwa imefika.

Askari polisi akiwa katika eneo la tukio.
“Sisi tulikuwa pale baa tunakunywa, mara tukamsikia mtu akipiga kelele za mwizi…mwiziii, ile kutoka ndiyo tukawaona hawa vijana wawili wakihangaika kuwasha bodaboda yao ili wakimbie.

“Yaani ilikuwa ni Mungu tu maana bodaboda isingegoma kuwaka, tusingewapata. Basi raia wenye hasira kali wakaanza kuwashushia kipigo, aliyekuwa akiendesha pamoja na yule dada aliyeibiwa wakachukuliwa hadi Kituo cha Polisi Mabatini huku aliyekwapua akipewa kipigo,” alisema shuhuda huyo.

Bodaboda iliyokuwa inatumiwa na vibaka hao ikiwaka moto baada ya kuchomwa na wananchi wenye hasira kali.
Hata hivyo, kijana huyo aliponea chupuchupu kuchomwa moto, kwani waliokuwa wamefuata mafuta ya petroli waliporudi walimkuta trafiki akizuia asiuawe.Kufuatia zuio hilo, raia hao walihamishia hasira zao kwenye kuichoma moto bodaboda kisha mtuhumiwa akachukuliwa hadi polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

»

ZITTO KABWE AMESHINDA NAFASI YA KIONGOZI MKUU WA- ACT WAZALENDO

Hongera sana ndugu zitto zuberi kabwe kwa kujinyakulia nafasi ya kiongozi mkuu, kazi iliyoko mbele yako ni kukitangaza chama kitaifa ili uweze kuwa na wabunge na mdaiwani-octoba 2015,Hakuna kazi kubwa kama kuwa kiongozi inahitaji busara na hekima ya hali juu

»

RAIS KIKWETE: SERIKALI HAITAANZISHA MAHAKAMA YA KADHI

Rais Kikwete amesema serikali haiwezi kuanzisha wala kuiendesha na kuihudumia Mahakama ya Kadhi na ameongeza kuwa hilo ni jukumu la Waislamu wenyewe na kwamba hawazuiliwi kuianzisha Mahakama hiyo na kwamba hayo ndio yalikuwa makubaliano.
Pia,Rais Kikwete amesema tamko la viongozi wa dini kuhusu suala la katiba mpya, limemshangaza, limemfedhehesha na kumsikitisha sana.
Rais Kikwete ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya amani cha viongozi wa dini wa mkoa wa Dar-es-salaam.
Chanzo: ITV

»

HIKI NDICHO CHANZO CHA KIFO CHA MWANZILISHI NA BOSI WA TIP TOP CONNECTION ABDUL BONGE

Abdu Bonge na Bab Tale 

Saa zinahesabika toka Tanzania na familia ya bongofleva ipokee taarifa za msiba wa Abdul Bonge Mwanzilishi wa kundi maarufu la Bongofleva Tiptop Connection lenye wanachama kama Tunda Man, Madee, Dogo Janja na wengine waliopita kama Keisha, Cassim Mnganga na MB Dogg.
Jioni ya March 28 2015 ndio taarifa zilianza kusambaa lakini chanzo cha kifo cha ghafla cha Abdul hakikuwa kimesemwa lakini mdogo wake ambae ni Babu Tale amesema 
>>> "Kuna mshkaji wetu mmoja alikua anagombana na mke wake jirani yetu, wakamfata hapa Abdul aende… mara ya kwanza na ya pili akakataa, mara ya tatu akasema ngoja aende’
‘Alivyoenda ukapita ukimya kidogo, baadae kuna mtu akaja kumuita kaka yetu mkubwa mwingine na kumwambia nenda kamsaidie kaka yako mkubwa amedondoka, kaka yangu baadae akanipigia simu akasema Bonge kama amezimia lakini sidhani kama atapona sababu wakati wa kuamulia ugomvi alianguka baada ya kusukumwa nafikiria aliangukia kichogo, kumpeleka Hospitali Manzese wakasema ameshafariki‘ – Babu Tale.

 Taarifa kutoka msibani leo March 29 2015 zinasema Abdul atasafirishwa kwenda kuzikwa Morogoro baada ya mwili kuzuiliwa leo mpaka uchunguzi ukamilike, kwa sasa Watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa bongofleva wako Tiptop Manzese kwenye kutoa pole, mwili unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Morogoro.

»

TCRA IZIMULIKE BLOGS ‘UCHWARA’ NA KUZICHUKULIA HATUA KALI‏


 
"Screen shot" ikionyesha moja ya habari zilizorushwa kwenye moja ya blog uchwara kuhusiana na taarifa za uzushi wa kifo cha mchungaji Gwajima.
…Ni zile zinazoandika habari za uongo, matusi
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Miongoni mwa mambo ambayo Tanzania tunapitia kwa sasa ni pamoja na teknolojia mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya simu, intaneti vyombo vya habari na mengine mengi, Lakini mawasiliano hayo kwa sasa ikiwemo Intaneti wapo wanayoyatumia vibaya.
Kupitia BLOG, mtandao ambao mtu anaweza kutengeneza chombo chake cha kutolea taarifa ama kufanyaia jambo lolote lile liwafikie wengi kwa mema, lakini kwa sasa hilo halipo kwani licha ya kuwa kila mtu anaweza kuanzisha blog imetoa mwanya kwa wengine kuzitumia blog hizo kinyume na matarajio.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na BLOG nyingi ambazo asilimia kubwa mtu yoyote anaweza kuanzisha tena bure kama ilivyo akaunti yako ya Email, watu wanaoziendesha BLOG hizo wamekuwa wakiongoza kwa kuweka habari za uongo, upotoshaji, habari zinazoenda kinyume na maadili, pamoja na habari ambazosi za kweli.
Tunaamini wapo watu wanaofanya shughuli hizi za BLOG, ambao ni Ma-blogger wazuri tu licha ya kuwa si wanahabari, lakini kwenye blog zao wana weka ‘POST’ habari nzuri na zinazoendana na maadili pia wamekuwa wakitoa habari za kuelimisha jamii, kuifunza jamii na wanapata wasomaji wanaotembelea wengi sana kiasi cha hata kupewa matangazo na baadhi ya Makampuni binafsi ya kibiashara, Serikali na watu wengine, lakini shida ni kwenye hizi ‘Blog uchwara’ ambazo kila kukicha wao kazi yao kukopi na ku-paste habari za kwenye magazeti na kuzipa ‘kiki’ kwenye blog zao wengine habari hizo hizo za kwenye magazeti wao kazi yao kubadilisha kichwa cha ‘habari tu ilimradi apate wasomaji wengi? Jamani kweli hii ni haki?, tena kichwa hicho cha habari hakiendani na maadili ya Mtanzania ama kinakiuka maadili hii si sawa, TCRA, muamke na kuchukua hatua kali.
1 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma.
Tunaamini Mamlaka yaa Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA),              (https://www.tcra.go.tz/) mpo na mnafuatilia lakini sijui kama mnaliona hili ni tatizo ama si tatizo.
Tukumbuke huko nyuma kulikuwa na mitandao kama hii tena ya watanzania ambao waliifungua ambapo walianza kuweka picha za kawaida na baadae ikawa inabadilika kuwa wanaweka picha za utupu… wakaachiwa hivi hivi baadae wakawa wanaweka picha za viongozi wakiwemo viongozi wakuu wa Nchi mwisho wa siku Mamlaka husika wakaja kukumbuka shuka wakati mambo yamekua si mambo.
Hivyo ni wakati sasa kwa TCRA, kuchukua hatua blog zote zinazoendana kinyume na maadili ikiwemo kupotosha, kuweka pichaa za ngono na kugombanisha watu basi zichukuliwe hatua.
Mtandao huu unaamini kuwa na unaungana na wadau wote wanaendelea kutoa maoni yao juu ya kuzitaka blog hizi zichukuliwe hatua. Kwani mpaka tunaandika habari hii ni pamoja na baada ya Mdau Yusuph Mhoja kuchukizwa na moja ya habari kwenye miongoni mwa blog hapa nchini. (Tazama picha), ambapo Mdau huyo aliuliza: “Hivi huyu mwandishi anajua kiswahili kweli? Yuko mochwari kwani amefariki huyo?” wakati anajiuliza hayo, hii ni kuwa inawatokea watu wengi sana wanaapokutana na habari kwenye hizo blog uchwara.
Wadau waliochangia mada ya Mhoja: Pendi Mahundi yeye alieleza hivi: “hahaha.... hili ndiyo tatizo kubwa la kila mtu mwenye kisimu cha TECNO bongo kujifanya blogger and a self-appointed journalist... UJINGA mtupu, huwa naziona habari kwenye viblogu mpaka kichefu chefu... full of attention-seeking sensationalism... utakuta heading: HATARI, Vilio na majonzi, Breaking news, Unbelievable..kisa tu kutaka watu wazisome blog zao.” Alieleza Mahundi.
Hata hivyo wachangiaji wengine waliomba serikali kupitisha mswada wa habari na sheria ya ICT ili kukomesha wandishi wa viblog uchwara.
IMG-20150310-WA0045 tunaamini pia Mtandao wa wanabloga Tanzania (Tanzania Blogger Network-TBN) wapo kwani kuna misemo mingi ya zamani inayosemwa, ikiwemo ule wa SAMAKI MMOJA AKIOZA…? Jibu watatupatiaa TBN ama kama si lao basi bomu likilipuka tusimtafute mchawi huko mbeleni.

»

RAIS KIKWETE “ABARIKI” MBIO ZA URAIS WA LOWASSA .....WAKUTANA KUJADILI KWA KIFICHO

SIRI imefichuka. Mbio za Edward Lowassa, kusaka urais kwa udi na uvumba, zimebarikiwa kwa asilimia 100 na Rais Jakaya Kikwete.
Lowassa amekutana na Kikwete mara kadhaa na kufunga makubaliano ya siri yanayolenga kumsaidia yeye kuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Yote yanayofanywa na Edward (Lowassa), yamebarikiwa na Kikwete. Bila hivyo, Lowassa asingekuwa na ubavu wa kufanya anachokitenda,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya serikali.
Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais wa Jamhuri.
Kuibuka kwa taarifa kuwa Lowassa amefunga makubaliano na Kikwete, kumekuja katika kipindi ambacho mwanasiasa huyo aliyeapa kufia katika vita ya kuwania madaraka, ameanza kupokea makundi ya wananchi akidai wanamuomba kugombea urais.

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, “Kikwete na Lowassa wanakutana sana, tena kwa siri. Wamejadili mengi, ikiwamo kinyang’anyiro cha urais. Itakuwa ajabu, bwana huyu kutokuwa mgombea kupitia CCM.”

Waziri mkuu huyo aliyejiuzulu kwa kashfa ya mkataba tata wa kufua umeme, kati ya serikali na kampuni ya Richmond, tayari amefungulia anaowaita “wafuasi wake,” kushawishi baadhi ya watu kwa lengo la kutafuta kila upenyo kuhakikisha anapata nafasi ya kushika utawala Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu walio karibu na mwanasiasa huyo, makubaliano yake na Kikwete ndiyo yanayomfanya kuwa “mbogo” hadi kuikuka taratibu za chama chake.
Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu – kuchagua rais, wabunge na madiwani.

Hata hivyo, mtoa taarifa wa MwanaHALISI Online anasema, pamoja na kuwapo makubaliano hayo, bado Lowassa hawezi kujihakikishia nafasi ya kuwa mgombea.
Anasema, Lowassa anakabiliwa na kibarua kigumu kutoka kwa makundi ya yaliyopachikwa jina la “wahafidhina” ndani ya chama chake.

»

ASKOFU GWAJIMA AZIMIA GHAFLA WAKATI AKIHOJIWA NA POLISI NA KUKIMBIZWA HOSPITALINI MUHIMBILI

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alizimia na kisha kukimbizwa hospitali wakati akihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Gwajima ambaye alijisalimisha kituoni hapo saa 8:22 jana mchana akiitikia wito wa polisi uliomtaka kufika kutokana na tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Waandishi wa Mtanzania Jumamosi waliokuwa kituoni hapo wanaeleza kuwa walimuona Gwajima akitolewa kutoka katika chumba cha mahojiano akiwa amebebwa.

Kwa mujibu wa waandishi hao Gwajima ambaye alikuwa amebebwa na maofisa wa polisi alipelekwa moja kwa moja kwenye gari aina ya Noah kwa ajili ya kumpeleka hospitali.

Tukio hilo lililotokea majira ya saa 3:16 usiku lilikuja katika kipindi kisichozidi dakika saba tangu askofu huyo alipoonekana akiwa ameshikiliwa na wasaidizi wake kuelekea msalani huku yeye mwenyewe akiwa amejishika kichwa.

Wakati akipelekwa hospitali, msafara wake ulikuwa ni wa magari mawili mojawapo likiwa ni aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili PT 1848 na Noah yenye namba za usajili T 215 BEM.

Akizungumza na gazeti hili kituoni hapo, mwanasheria wa askofu huyo, John Mallya alisema wakati wakiwa katika mahojiano, alisema anahisi kizunguzungu na baadaye akaishiwa nguvu na akawa amefumba macho.

Mallya alisema baada ya hali hiyo kutokea, polisi walimchukua na kisha kumpeleka katika hospitali ya Jeshi la Polisi iliyoko Kurasini, Dar es Salaam.

Wakati Mallya akiwasiliana na gazeti hili majira ya 4:30 usiku alisema kuwa walikuwa wakifanya mchakato wa kumuhamishia katika hospitali ya TMJ kutokana na yake kutokuwa nzuri.

“Siwezi kujua tatizo ni nini na siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo maana hayo ni mambo ya kitabibu” alisema Malya.

Ilipotimu saa 4:41 Waandishi wa gazeti hili ambao nao walifika katika hospitali hiyo ya Jeshi la Polisi walishuhudia Gwajima akitolewa katika hospitali hiyo ya Jeshi la Polisi na kisha kupakizwa katika gari maalum la kubebea wagonjwa lenye namba DFP 6309.

Wakati hayo yakitokea taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili zilidai kuwa; kwa muda wote akiwa katika mahojiano, Gwajima alikuwa hajala chochote hali ambayo iliibua wasiwasi kwamba huenda ilichangia kubadilika kwa afya yake.

Polisi mmoja aliyekuwa katika chumba cha mahojiano aliwaeleza waandishi wetu kwamba Askofu Gwajima alipoteza fahamu muda mfupi baada ya kuhojiwa kuhusu mali anazozimiliki.

Awali wakati Gwajima alipowasili kituoni hapo mchana kabla ya kuhojiwa alizungumza na waandishi wa habari ambapo alikiri kutoa lugha chafu dhidi Kardinali Pengo.

Gwajima ambaye alifika kituoni hapo saa 8:22 mchana alisema kauli yake hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii aliitoa kutokana na Kardinali Pengo kuwageuka wenzake ambao ni Baraza la Maaskofu Tanzania linalounganisha Wakatoliki, Pentekoste na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kukubaliana kwa pamoja kuwa hawataki Mahakama ya Kadhi.

Alisema maaskofu wote walikubaliana kuhusu tamko hilo na kisha kulisaini lakini anamshangaa Kardinali Pengo ambaye pia alisaini kuwageuka.

“Mimi kama kiongozi wa kiroho nikaona nimkemee kiongozi mwenzangu wa kiroho aache mambo ambayo si mazuri. Hakuna maneno ya kashfa ambayo nimeyatoa. Niliyotoa ni neno la Mungu linalotumiwa kumwongoza mtumishi wa Mungu,” alisema Gwajima.

Alisema anashangaa kuitwa polisi kwani hajatukana polisi na ndio sababu akaitika wito na kufika.

Gwajima alifika polisi akitembea kwa miguu kutokana na foleni kali iliyokuwepo barabarani huku akiwa ameongozana na Mwanasheria wake John Malya pamoja na baadhi ya wachungaji, waumini wa kanisa hilo na wengine waliotajwa kuwa ni walinzi wake.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Suleimani Kova alisema Mchungaji Gwajima ametii amri ya Jeshi hilo kama alivyotakiwa.

Kova alisema baada ya kufika kituoni hapo alielekezwa kwenda kumuona Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP Costantine Massawe.

Akitaja tuhuma zinazomkabili Mchungaji Gwajima, Kova alisema ni pamoja na kumkashifu na kumtukana hadharani kiongozi wa Kanisa Katoliki Kardinali Pengo.

“Taratibu za kuhojiwa zimeshaanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa atapewa haki zote anazostahili ikiwemo kuwa na ndugu yake wa karibu, rafiki anayemwamini au wakili wake. Kama ilivyokawaida utakusanywa ushahidi kutoka pande zote za shauri hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio hilo lilivyotokea,” alisema Kova.

Kova alisema baada ya hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya kitaalamu na ya kisheria ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka.

“Ili ufanisi upatikane katika upelelezi wa shauri hili ni muhimu kupata ushirikiano kutoka kwa kila atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha haraka upelelezi wa shauri hilo ambalo limepata mvuto mkubwa kwenye jamii,” alisema Kova.

Katika video na sauti zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa What’s App, Gwajima alirekodiwa akiwa kwenye ibada ya kanisa lake akitumia lugha zisizokuwa na staa kwa Kardinali Pengo akimtuhumu kuwa ni msaliti kwani amekwenda kinyume na Taasisi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kuwataka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa kisha wapewe uhuru wa kupiga kura ya “ndiyo” au “hapana” tofauti na vyombo hivyo vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo vilivyotaka waumini waipigie kura ya “hapana”.

»

ALIYEKUWA MKE WA MH MBUNGE SUGU FAIZA ALLY ATANGAZA MTANDAONI KUWA ANA HAMU YA KUFANYA MAPENZI

Wadau nashindwa kuelewa kwanini tuna jikuta tunaingia kwenye mahusiano ya kipuuzi namna hii hivi kweli ni maadili ya afrika ndo yamefikia huku kweli jaman mke wa mbunge wa mbeya ,mjini sugu anatangaza mtandaoni kua ana hamu ya kufanya mapenzi na kuona hii hali ni ya kwaida kwake watu tusishituke kabisa

Soma Alichoandika Hapa Chini :

"Natamani sana kufanya Sex nikikwambia Nina muda gani sijafanya huwezi kuamini-I NEED SEX # GOOD ONE "


Toa Maoni yako kuhusu Faiza Ally Kutangaza kuwa Ana hamu ya Ku do....

»

USHAURI WA BURE KWENU WANAWAKE MABUBU NA MAGOGO KUNAKO KITANDANI

Raha ya mapenzi ni kuridhishana na kufikishana kunako kilele cha utamu.Hakuna faida ya kua na mpenzi ambae kunako 6*6 hakuna lolote analo lijua zaidi ya kuchoshana tu na kupakana jasho.Ili uweze kumlizisha mwenza wako sio lazima mfanye mapenzi kwa mda mrefu au sio lazima mpaka mwanaume amiliki dushe la inchi 7.Mwanaume wa ukweli ni yule ambae anaweza kucheza na maeneo muhimu ya utamu ya mwanamke.

Na mwanamke wa ukweli ni yule ambae anaweza kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mwanaume wake wakati wa tendo la kugegedana.Hata kama mwanaume una kibamia chako cha inchi3 haijalishi.Ndani ya nusu saa tu unaweza kumlizisha mpenzi wako kama unayajua vizuri maeneo muhimu ya utamu wa mwanamke na jinsi ya kuyapata na kuyakuna vizuri.

Kwa bahati nzuri wanawake wana maeneo matano(5) muhimu ambayo uwawezesha kusikia utamu wakati wa kugegedanaSehemu muhimu ni;

(1)mwanzo wa papuchi(mdomoni)

(2)kuta za papuchi

(3)kisimile(clitoris)*

(4)Kipele G(G Spot)

(5)AFE (mwisho kabisa mwa kina cha papuchi)

Mwanamke anaweza kufurahia kupata utamu wa tendo hili takatifu la kugegedana kwenye maeneo hayo muhimu kama mwanaume anajua kuwajibika na ni mtundu wa kucheza na maeneo muhimu tu.Haijalishi unatumia mda gani na unamiliki dushe la saizi gani.

Lakini utamu wa maeneo hayo muhimu unazidiana.Kwahiyo katika maeneo hayo eneo namba nne(3) na namba tano(4) ndio maeneo muhimu sana kuliko maeneo hayo mengine na mwanaume anatakiwa awe mtaalamu wa kutumia dushe lake vizuri kugusa hayo maeneo muhimu

Ushauri kwa wanawake Mabubu:
Mwanamke unatakiwa uwe huru na wazi kumueleza mwanaume wako ikiwa kagusa kusiko au kapatia kunako utamu.Haipendezi kwa mtoto wa kike kua bubu kama vile umepigwa na shoti ya umeme.Na unapoguswa sehemu muhimu mueleze kwa maneno kua apoapo umepatia,au toa sauti ya mahaba,legeza macho,likatikie dushe ili kumpa moyo mwanaume wako na aendelee kukukuna vizuri.Sio unabaki umeshupaa uso na hata kuguna kidogo huwezi kama vile ulilazimishwa kugegedwa wakati ulikubali mwenyewe.

Mwanaume unatakiwa ujue maumbile ya dushe lako na ujue ni staili gani nzuri itakayokufanya uweze kuzipata hizo sehemu muhimu kwa urahishi.Na hakikisha unapopiga nje ndani basi dushe lako halikosi shabaha ya kulenga vizuri kile kipeleG kwababu ndio utamu wenyewe wa mwanamke unapopatikana.Staili ya doggy staili/chuma mboga/mbuzi kagoma ambazo wanaume wengi wanazipenda ni nzuri kwa mwanaume kwasababu ya kupigwapigwa na yale makalio lakini ni ngumu kuweza kukipata kipeleG kwa urahisi.Kwahiyo unashauriwa kuzifanya mwishoni wakati tayari umeshamridhisha mpenzi wako

Ushauri kwa wanawake Magogo:
Jitahidini kufanya mazoezi ya viungo ili muwe wanyumbulifu na muweze kuwa wepesi wa kumudu staili tofautitofauti.Ili umsaidie mwanaume wako aweze kukugusa sehemu zako muhimu na kukufikisha kunako kilele cha utamu.Wapo wanawake wengine wanadhani kumudu staili tofauti tofauti ni umalaya lakini dhana hii sio ya kweli.Mtoto wa kike unatakiwa kua mbunifu sio tu kuendekeza staili moja tu ya kifo cha mende.Kila unapopanda kwenye uwanja wa 6*6 huna chochote unachojua zaidi ya kutenga bakuli tu.Ni aibu sana kwa mtoto wa kike kukakamaa kama ubao na na husitafute mchawi ukiachika.

Kwa leo yangu ni hayo tu nawaachia wadau wengine kuongezea mengine


N.B (*)-tafsida kidogo imetumika ili kupunguza ukali wa neno

»

NAY WA MITEGO AFANYA KWELI, APIMA DNA YA KUDHIBITISHA KUWA MTOTO NI WAKE AMA LA, MAJIBU KUTOKA MWEZI WA NNE

Mwimbaji Nay wa Mitego ametimiza ahadi aliyosema kuwa atapima DNA kujua kama kweli mtoto aliyezaa na Siwema ni wake ama la baada ya Siwema kudai kuwa mtoto huyo si wake bali ni wa Obasanjo....

Nay wa Mitego amehabarisha kuwa Amepima DNA kwa Mwanakemia mkuu na Kuambiwa kuwa majibu yatatoka mwezi wa nne tarehe 8 ......

Kila la Heri Bwana Nay

»

STELLA TILLYA AKA CHAGGA BARBIE ADAI MIMBA YA ZARI SI YA DIAMOND BALI NI YA MR KATUNZI..DIAMOND ANALEA TU

In the on going battle between Zari and Chagga Barbie it has been revealed that Zari’s pregnancy is not Diamond’s! Chagga Barbie wrote to remind Zari that she is carrying a baby for a man she named by one name ‘Katunzi’

This message comes from a lady known as Stella Tillya or Chagga Barbie but due to some circumstances she calls herself Muke ya Muganda. Stella is a Tanzanian Socialite in USA.

»

UNYAMA GANI HUU:MWANAMKE ANUSURIKA KUCHINJWA NA MWANAMKE MWENZAKE

Wanawake wanne wanaojiita Kundi la ‘Boko Aramu, hivi karibuni wamemteka msichana mmoja mrembo aitwaye Marry kisha kumfanyia kitu mbaya ikiwa ni pamoja na kumdhuru sehemu zake za siri.
Marry akiwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kunusurika kuchinjwa.
Sikia simulizi ya Marry
Akizungumza kwa tabu akiwa katika Hospitali ya Mount Meru, Marry ambaye anamiliki saluni ya kike alisema, chanzo cha kufanyiwa hivyo ni wivu wa mapenzi huku akimtaja rafiki yake wa karibu aitwaye Maurin kuhusika.
Alisema, siku ya tukio akiwa ndani ya saluni yake alifika Maurin na kumtaka aende kwenye chumba chake kuna jambo akamsaidie lakini alipofika huko akashangaa anataitiwa.
“Ilikuwa saa mbili usiku, alikuja Maurin na kuniomba niende katika chumba chake, nilipofika tu mlangoni kwake akanisukumia kitandani, mara nikaona kundi la wanawake likinivamia na kuanza kunishambulia.
“Walinipiga sana, baadaye walinivua nguo zote na kunilaza kitandani kisha mmoja akanifanyika kitendo cha kikatili ambacho siwezi hata kukisimulia.

Baadhi ya ndugu wa Marry wakiwa katika kituo cha polisi.
Niliumia sana, nikapiga kelele sana lakini hawakuniachia,” alisema Marry na kuongeza:
“Walizidi kunikandamiza, nahisi lengo lao ilikuwa ni kuniua. Mara mwanamke mmoja akaniuliza kwa nini natembea na bwana wa Maurin. Nikashangaa kusikia maneno hayo. Nikawaambia Maurin ni rafiki yangu na wala huyo bwana wake simjui. Basi wakazidi kunipiga.
“Mmoja akachukua kisu na kuniwekea shingoni, mwingine akachukua kichupa ambacho nahisi kilikuwa na tindikali, ikabidi nijilazimishe kuamka na kuwapigia magoti wasiniue.“Wakakubali kunisamahe lakini wakadai niwalipe gharama zao kwani wametoka Dar kuja kuniua. Nikawaambia sikuwa na fedha, wakaitana pembeni kisha wakaondoka na kuniacha pale nikiwa na maumivu.
“Walipoondoka tu nikaanza kupiga kelele na ndipo watu walipokuja kunipa msaada kisha tukaenda kutoa taarifa katika kituo kikuu cha polisi na kufungua jalada la kesi lenye namba AR /RB /3717/2015,” alisema Marry.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Edward Balele alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mpaka sasa jeshi hilo linawashikilia wanawake wawili kati ya wanne waliohusika kumtendea unyama dada huyo.

»